TANZANIA YAIOMBA KOICA KUONGEZA MUDA WA MKATABA WA MRADI WA GEBR
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati)
akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdula Lutavi (aliyeipa
mgongo kamera) wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo
pichani) kwa ajili ya kufungua Kongamano la pili la kimataifa la uchumi
endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini,
kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara
linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort, Mkoani Tanga. Kulia
ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika,
Firmin Matoko. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Kongamano
la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira
kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu
Kusini mwa Jangwa la Sahara (GEBR) limefanyika mkoani Tanga.
Wenyeji
wa kongamano hilo walikuwa ni Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
sayansi na Utamaduni (UNESCO) ofisi ya Dar es salaam.
Akifungua
kongamano hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia
Suluhu Hassan ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Korea kusini kupitia
shirika lake la maendeleo na ushirikiano la kimataifa (KOICA) kuongeza
muda wa mkataba wa mradi wa GEBR ambao unafikia ukomo mwishoni mwa mwaka
huu.
Akizungumza
na washiriki mbalimbali wapatao 40 kutokana ndani na nje ya nchi
zikiwemo Ghana na Nigeria kutoka Afrika, alisema ombi hilo linatokana na
ukweli kuwa walengwa wamekuwa wakifaidika na mradi huo, kwa kuweza
kubadilisha maisha yao na kuwa bora zaidi.
Makamu
wa Rais alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na
kutoweka kwa uotoasili unaotoa fursa ya uoto wa mimea zaidi ya 10,000,
jamii 6,000 ya wadudu, jamii ipatayo 1000 ya ndege warukao.
Aidha
Samia katika hotuba yake alirejea msimamo wa serikali wa kutaka
kuhifadhi mazingira, pamoja na kuziweka rasmi chini ya uangalizi halali
jumla ya hekta milioni 33.5 za misitu asili, huku akitanabaisha kuwa
serikali pia ina mapori ya akiba yapatayo 800 pamoja na misitu mingine.
Aliwakumbusha
washikadau pamoja na nchi wafadhili kwamba Tanzania inakabiliwa na
ukuaji mkubwa wa idadi ya watu wake wanaotegemea raslimali kwa matumizi
yao ya kila siku pamoja na mahitaji ya nishati.
“Tunaelewa
kwamba kuna shughuli nyingi za uharibifu wa mazingira zinazopelekea
uharibifu wa misitu na mazingira”, alisema Samia na kuongeza kwamba kuna
kupokonyana kwa ardhi na maji.
Katika
warsha hiyo wafaidika wakubwa katika mradi huo, ambao walitekeleza kwa
vitendo elimu iliyopatikana kutokana na mradi huo, walikabidhiwa vyeti
ya ushiriki kwa vitendo na kwa ufanisi mkubwa walioonyesha.
Washiriki
hao wengi walitoka katika miradi midogo midogo inayotekelezwa Amani,
Muheza ambayo ni pamoja na ufugaji nyuki, samaki, vipepeo na uyoga.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
nchini, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) alipowasili kwenye hoteli ya Tanga
Beach Resort jana kufungua Kongamano la pili la kimataifa la uchumi
endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini,
kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara
lililoandaliwa na UNESCO. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais, Mhandisi Ngosi Mwihava.
Awali,
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza aliwataka wakazi wa Tanga na
Tanzania kwa ujumla kutumia vyema nafasi adhimu kwenye miradi ya
maendeleo inayogharimiwa na wafadhili na kuwasihi wawe makini kwani
mafanikio yao huwa ni kivutio kwa wafadhili kuweza kuendelea kutoa
ufadhili kwa misaada.
Mradi
wa GEBR ambao uko katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wake,
unafadhiliwa na serikali ya Korea kupitia Shirika lake la Kimataifa la
misaada Korea International Cooperation Agency (KOICA).
Mradi huo wa Unesco wa binadamu na bayosfia (MAB) unatekelezwa nchini Ghana, Nigeria na Tanzania kwenye milima ya Usambara.
Katika
hotuba yake Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika, Firmin
Matoko alimpongeza Makamu wa rais kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika
nafasi ya juu katika utawala tangu historia ya kuundwa kwa Tanzania.
Alisema amefurahishwa sana na wanawake kuchukua nafasi kwa kuwa Unesco wameweka kipaumbele wanawake katika maendeleo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano hoteli ya Tanga Beach Resort akiwa
ameambatana na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko.
Akizungumzia mradi wa GEBR alisema umelenga kutekelezwa katia msingi wa wazo la UNESCO la binadamu na bayosfia.
Alisema
kwamba mradi huo umelenga kutumia elimu ya asili, elimu ya sayansi na
utamaduni ili kuboresha maisha ya biandamu huku wakihifadhi mazingira.
Aidha
alitaka kuwapo ushirikiano katika utekelezaji wa ajenda za maendeleo na
hifadhi ya bayosfia kwa lengo la kuwezesha maendeleo endelevu.
Washiriki wa mradi huo pia walipata nafasi ya kutembelea eneo la hifadhi ya Usambara mashariki.
Naye
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Bw Geum-Young Song alisema kwamba
wataendelea kushiriki katika mradi huo ambao umejikita katika kuwezesha
maendeleo endelevu huku mazingira yakihifadhiwa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua
Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuai katika
hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo
endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo limefunguliwa
Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani
Tanga.
Alisema ni lengo la taifa lake la kuwezesha hifadhi endelevu kwa maendeleo endelevu.
Aidha alitaka kuwepo na fikra za mradi kuwa endelevu baada ya wafadhili kuondoka.
Viongozi
waliohudhuria siku ya ufunguzi ni pamoja na Makamu wa Rais Tanzania,
Mh. Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya
Afrika, Bw. Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania,
Mh. Geum -Young Song, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Unesco nchini
Tanzania, Zulmira Rodrigues, Wawakilishi wa KOICA nchini Ghana, Nigeria
na Tanzania; mwakilishi wa KOICA nchini Korea, Seoul; na kamati za MAB
kutoka nchi zinazotekeleza mradi huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akifungua Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuwai
katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na
maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo
limefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach
Resort Mkoani Tanga.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Afrika, Firmin Matoko kuhutubia kwenye kongamano
hilo.
Mkurugenzi
Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UNESCO, Irina Bokova wakati
wa ufunguzi wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu
unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda
bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea
katika hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Balozi
wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song ambao ni wafadhili wa
mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui akisoma taarifa yake
baada ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan, kufungua Kongamano hilo la pili la Kimataifa
inayojadili kuhusu Bayoanuai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na
uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la
Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa
Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Pichani
juu na chini washiriki wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi
endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini,
kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara
linaloendelea katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani
Tanga.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Uyoga (DMGA), Bi
Judith Simon Muro, kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye
kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi cheti Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira asili Amani (Amani
Forest Nature Reserve – ANR), Bi. Mwanaidi Kijazi, kwa kutambua
mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa
kulinda Bayoanui. Wanaoshuhudia tukio hilo kulia Mkurugenzi Mkuu
Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri
ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song (wa pili kushoto) pamoja na
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda
na Burundi, Bi. Mary Kawar (wa kwanza kushoto).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi cheti Amiri Saidi Sheghembe wa mradi wa Vipepeo Amani kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda Bayoanui.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ,
akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania,
Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar.
Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia
Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na washiriki kutoka nje ya Tanzania
wanaohudhuria Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu
unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda
bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea
katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia
Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la pili
la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia
ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini
mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia
Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa UNESCO
walioshiriki kwenye maandalizi ya kongamano hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akiteta jambo na Afisa Tathimini na Logistki wa UNESCO Ofisi ya Dar es
Salaam, Rahma Islem (kulia) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
Mkurugenzi
Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko (kushoto)
akisalimiana na mmoja wadau wa maendeleo Balozi wa Jamhuri ya Korea
nchini, Mh. Geum-Young Song .
No comments:
Post a Comment