Tuesday, February 28, 2017

MEYA JIJI LA TANGA APIGA MARUFUKU UVAAJI WA JEANZ NA NGUO AMBAZO HAZINA STAHA



Tanga, MEYA wa jiji la Tanga, Mustapha Mhina, amepiga marufuku uvaaji wa suruali aina ya jeanzi wakati wa vikao vya baraza na kuwataka kuheshimu vyenginevyo kanuni za baraza kwa kuwatoa nje.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani jana, Mhina alisema ni marufuku kuvaa suruali aina ya jeanzi pamoja na mavazi mengine ambayo hayana staha ndani ya baraza.
Alisema kwa muda mrefu amekuwa akioona tabia hiyo na kuivumilia jambo ambalo amelichunguza hakuna mabadiliko hivyo kanuni za baraza zitafanya kazi bila ya kuonea mtu hutuma wala sura.
“Waheshimiwa madiwani mwisho leo kumuona diwani amevaa suruali aina ya jeanzi au mavazi ambayo hayana staha si kwa wanawake wala wanaume” alisema Mhina na kuongeza
“Hiki ni chombo kinatakiwa kuheshimiwa na kila mjumbe wa baraza hili natoa angalizo mapema kikao kijacho kabla ya kuanza kwa baraza nafanya ukaguzi” alisema
Alisema kuanzia sasa atakuwa mkali kwa kila jambo ambalo ataliona haliko sawa ndani ya baraza ikiwemo kufika kwa wakati ndani ya baraza na utoro ambao hautakuwa na taarifa.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Maweni , Joseph Collivas (CCM) amewataka wajumbe wa baraza la madiwani kutoa kero za wananchi katika maeneo yao na kuyapatia ufumbuzi wa haraka.
Alisema kuna changamoto nyingi katika maeneo ambayo madiwani wanawakilisha lakini hadi muda wa sasa hakuna hatua zozote ambazo zimepatiwa ufumbuzi ikiwemo mrefeji wa maji eneo la stendi kuu ya mabasi ya Kande ambayo hayana uelekeo.
“Madiwani wenzangu hebu tujadilini kero za wananchi ambao wametuchagua na kuyapatia ufumbuzi, kila mmoja kwake kuna kero kama sio dampo kuna migogoro iwe ya mipaka au ya viwanja” alisema
Aliwataka madiwnai hao kuhakikisha wanavitumia vikao hivyo kwa manufaa kwa wananchi bila kuangalia chama kwa madai kuwa kinachotakiwa ni maendeleo ya wananchi.
                                                     Mwisho
.


Meya wa jiji la Tanga, Mustafa Mhina (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa jiji la Tanga, Daudi Mayeji wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani

AMKA NA MAGAZETI NA FREYS LUXURY BUS TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU



RHINO CEMENT TANGA YAKABIDHI MADAWATI 350 SHULE MSINGI KANGE TANGA



Tanga, MKUU wa  Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa, amekishukuru kiwanda cha Saruji cha Rhino  cha Tanga kwa msaada wake wa madawati 350 kwa shule ya Msingi ya Kange na mabenchi 10 kwa Zahanati iliyopo ndani ya kata hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano, Mwalapwa alisema msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi darasani kukaa chini hivyo kutaka makampuni mengine kufuata nyayo za kiwanda hicho cha Rhino.
Amesema mabenchi 10 kwa Zahanati pia itaondosha kero kwa wagonjwa wanaofika kituoni na kuondosha kero ya foleni ya kukaa chini kusubiri huduma.
“Niseme kutoka moyoni nimepata faraja kubwa kwa ndugu zetu kutukumbuka jiwe moja kwa ndege wawili, madawati 350 kwa shule na mabenchi 10 kwa Zahanati, hili ni tukio jema la faraja” alisema Mwailapwa
Kwa upande wake Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rhino, Girish Gumar, amesema msaada huo wa madawati 350 na mabenchi kwa Zahanati uko na thamani zaidi ya milioni 45.
Alisema kiwanda cha Rhino kimekuwa kikisaidia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Afya, Mazingira na huduma nyengine za kijamii.  



Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rinho, Girish Kumar akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa moja ya madawati 350 kwa shule ya msingi ya Kange  kupunguza kero ya uhaba wa madawati kwa shule hiyo ambayo awali wanafunzi walikuwa wakisomea chini.









 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange  Tanga wakipeleka madawati madarasani kati ya madawati  350 yaliyotolewa  na kiwanda cha Saruji cha Rinho jana. Shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa madawati na baadhi ya wanafunzi kulazimika kukaa chini