Hivi ndivyo Whatsapp imevunja ndoa ya wawili hawa…
Mwanaume mmoja Saudi Arabia ametoa
talaka kwa mkewe kutokana na kitendo cha mwanamke huyo kutokujibu
message aliyomtumia WhatsApp.
Mwanaume huyo amesema kitendo
kilichomkasirisha zaidi ni pale aliporudi nyumbani na kumkuta mke wake
akiwa busy anachat na marafiki zake kupitia mtandao huo wakati message
aliyomtumia yeye hakuijibu.
Jamaa huyo ameona kama kitendo hicho ni
dharau kubwa na hakuwa tayari kuendelea na ndoa hiyo ambayo imedumu kwa
miaka miwili tangu ifungwe.
No comments:
Post a Comment