Yahya Jammeh ameondoka Gambia na kuelekea Guinea
Hapo jana Jammeh alitangaza kwamba atang'atuka baada kuongozi Gambia kwa miaka 22.
Kwa mujibu wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi ECOWAS, Jammeh amewasili nchini Guinea . Siku ya Alhamisi ECOWAS illituma vikosi vyake nchini Gambia kumshurutisha Jammeh kukubali Adama Barrow aapishwe.
Jumuiya hiyo inasema imesitisha oparesheni yake ya kijeshi Gambia lakini wanajeshi elfu saba watasalia nchini humo kudumisha usalama, huku Adama Barrow akitarajiwa kurejea Gambia kutoka nchi jirani ya Senegal muda mfupi ujao.
No comments:
Post a Comment