VIONGOZI WALIOPORA MAMILIONI YA FEDHA WAKIWA MADARAKANI
Viongozi waliopora nchi zao mamilioni ya pesa wakiwa madarakani.
Zaidi ya dola
milioni 11 zinaripotiwa kutoweka kutoka kwa hazina ya taifa nchini
Gambia, kufuatia kuondoka kwa kiongozi wa muda mrefu Yahya Jammeh.
Jammeh alikwamia madaraka kwa karibu miezi miwili licha ya kushindwa kwenye uchaguzi wa urais mwezi Disemba.
Jammeh ambaye kwa sasa yuko nchini Equatorial Guinea, si kiongozi wa
kwanza anayelaumiwa kwa kupora pesa za umma. Kuna wale walipora nyingi
zaidi na hawa ni baadhi yao. Sani Abacha, Nigeria Sani Abacha, kiongozi wa Nigeria kutoka mwaka 1993
hadi 1998, aliripotiwa kupora kati ya dola bilioni moja na bilioni 5
kutoka kwa hazina ya taifa. Mwaka 2014 idara ya haki nchini Marekani
ilisema kuwa ilitwaa mali ya Abacha yaliyokuwa yameibwa ya thamani ya
dola milioni 450. Suharto, Indonesia Suharto, rais wa Indonesia kutoka mwaka 1967 hadi
mwaka 1998, anadaiwa kuisafisha hazina ya taifa ya nchi kwa hadi dola
bilioni 35. Mwaka 2000 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani na
kushtakiwa kwa kuiba dola milioni 570. Lakini madaktari waligundu kuwa
alikuwa mgonja sana kuweza kufika mahakamani . Aliaga dunia mwaka 2000 . Mobutu Sese Seko, Zaire Kiongozi wa Zaire ambayo sasa ni Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo kutoka mwaka 1965 hadi mwaka 1997, Mobutu aliongoza
utawala dhalimu ambao ulikandamiza upinzani. Pia aliishi maisha ya anasa
na kujirundikia mali nyingi ikiwemo nyuma ya viumba 30 huko Lausanne ya
thamani ya dola milioni 5.5. Anakisiwa kuiba dola bilioni 5. Ferdinand Marcos, Ufilipino Mke wa Marcos, Imelda alikuwa na viatu 3000. Marcos
anaaminiwa kuiba dola bilioni 10 akiwa madarakani kati ya mwaka 1965 na
1986. Baada ya kifo chake kesi kadha ziliilazimisha Uswizi ambapo
alificha pesa hizo kurudisha karibu dola milioni 7000 kwa utawala wa
Ufilipino. Ali Abdullah Saleh, Yemen Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh anakisiwa
kupora karibu dola milioni 60 wakati akiwa ofisini. Aliondolewa
madarakani mwaka 2012 wakati wa mapinduzi ya nchi za kiarabu lakini sasa
anashirikiana na waasi wa Houthi katika nchi hiyo iliyokumbwa na
mapigano. Slobodan Milosevic, Serbia Slobodan Milosevic, Ni kiongozi dhalimu ambaye
aliitawala Serbia kati ya mwaka 1989 na 1997. Alishtakiwa kwanza kwa
kuendesha mauaji ya halaiki. Lakini pia alishtakiwa kwa kupora pesa za
umma. Kiwango alichopora hakijulikani lakini anakisiwa kuiba kati ya
dola bilioni 1 na bilioni 4. Aliaga dunia mwaka 2006 akiwa kwenye
mahakama ya Hague. Hosni Mubarak, Misri Alipinduliwa mwaka 2011. Hosni mubarak alishtakiwa
kwa kuiba pesa zilizonuiwa kukarabati ikulu za rais na kuzitumia kujenga
miradi yake binafsi. Mubarak na wanawe wa kiume walipatikana na hatia
ya kuiba zaidi ya milioni dola 17 kati kipindi cha miaka minane.
Alihukumiwa kifungi cha miaka mitatu jela huku wanawe wakihukumiwa
kifungo cha miaka minne kila mmoja. Ben Ali, Tunisia Mwaka 2011 wakati wa kupinduliwa kwa Ben Ali,
yalianza mapinduzi ya nchi za kiarabu. Ali na mkewe walikimbia kwenda
Saudi Arabia lakini mahakama ya Tunisia iliwahukumu bila ya wao kuwepo
kifungo cha miaka 35 jela kwa kupora pesa za umma. Wakati wa kesi yao
mwendesha mashataka alisema kuwa vito vya thamani ya dola milioni 27 na
pesa vilipatikana ndani ya moja ya nyumba zao.
BBC
No comments:
Post a Comment