Floyd Mayweather amestaafu? Kati ya hawa saba, mmoja anamsubiri Ulingoni kufunga nae hesabu..
Baada ya Pambano la Floyd Mayweather VS Andre Berto ambalo walipigana usiku wa kuamkia September 13 2015, Mayweather aliongea kauli hii >>> ‘Nimekamilisha
kila kitu, nimefanya kila kitu kwenye mchezo wangu… Umri wangu
unakaribia miaka 40, hakuna nilichobakiza kwenye Ulimwengu wa Ngumi,
nahitaji kutumia muda mwingi zaidi na familia yangu‘>> hii ilikuwa ni uthibitisho wake kwamba yeye na masuala ya Boxing ndio yamefikia mwisho !!
Nje ya Ulingo stori ziko nyingi sana, japo watu wengi hawakuvutiwa na Pambalo kati ya Mayweather na Berto kutokana na kupishana kwa Rekodi zao, kuna list ambayo imepangwa na Wachambuzi wa mambo wanasema Floyd Mayweather hawezi
kuishia kuandika Rekodi ya kushinda mapambano 49, wanasema lazima jamaa
ataongeza pambano moja ambalo akishinda atakuwa ameandika Rekodi ya
kucheza Mapambano 50 na kushinda yote ndani ya kipindi cha miaka 19
ambayo amekuwa Bondia.
Hapo ni Miguel Cotto na Canelo Alvarez, ishu iko hivi.. hawa jamaa wana pambano November 21 2015 Las Vegas Marekani, mshindi kati yao huenda akakutana na Mayweather kwenye Pambano linalofatia. Cotto ni Bondia anayesimamiwa na Kampuni ya Jay Z, Roc Nation Sports.
Emmanuel “Manny” Dapidran Pacquiao, Bondia Mfilipino ambae alisafiri kwenda Marekani na akapigwa na Mayweather… macho ya wengi ni kuona marudio ya Pambano hilo ambalo lilivunja Rekodi kuwa na mauzo makubwa ya Ticket, Pacquiao kaingia pia kwenye list ya wanaotarajiwa kupambana na jamaa kwenye Pambano lijalo.
Danny Garcia,
jamaa ana Rekodi nzuri pia ya kushinda Mapambano 31 na hajapigwa
Pambano hata moja, kati ya Mapambano hayo.. 18 ameshinda kwa Knockouts…
Nae kaingia kwenye list ya wanaosubiri maamuzi ya Mayweather kurudi tena Ulingoni.
Amir Khan,
Bondia wa Uingereza mwenye Rekodi ya kucheza Mapambano 31 lakini kati
ya hayo alipigwa kwenye Mapambano matatu tu. Huyu nae yumo kwenye list
ya Mayweather.
Keith Thurman,
jamaa nae ana rekodi ya nguvu yani.. kacheza Mapambano 26 na kashinda
yote, unaambiwa kwenye Ushindi wake ana Mapambano 22 aliyoshinda kwa
knockouts. Huenda ikawa Mayweather VS Thurman pia pambalo lijalo.
Kell Brook, Rekodi yake ni nzuri pia.. ana jumla ya Mapambano 35 ambayo yote kashinda, na Mapambano 24 kapata ushindi kwa knockouts.
Mbabe mwingine ndio huyu mtu wangu, anaitwa Gennady Golovkin…
Rekodi ya ubabe wake inadhihirishwa kwenye Mapambano 33 aliyowahi
kucheza, unaambiwa ameshinda yote na kati ya hayo, Mapambano 30
kayamaliza kwa ushindi wa knockouts.
Floyd ‘Money’ Mayweather anarudi
Ulingoni? swali jingine ni kwamba anarudi na nani kati ya hawa wenye
Rekodi za nguvu kabisa? Atafanikiwa kuandika Rekodi ya Ushindi kwenye
Pambano la 50?
Majibu yatapatikana soon, kama pambano
hili likithibitishwa basi story huenda ikawa kubwa pamoja na promo ya
nguvu ambayo inaweza kufananishwa na Rekodi ya mauzo makubwa
yaliyofanyika kabla ya Pambano la May 02 2015, Floyd Mayweather VS Manny Pacquiao..
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment