Ethiopia wameanza rasmi kutumia Treni za abiria zinazotumia umeme.

Ripoti
inasema Treni hizi ambazo zimezinduliwa September 20 2015 zinaanza
kubeba abiria na zinatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa watu kwenye
mji mkuu wa
Addis Ababa,
Ethiopia nchi ambayo mpaka mwaka huu wanasema idadi ya watu wake ni zaidi ya
MILIONI 90.

BBC
wanasema hizi Treni zimetajwa kuwa mfano na za kwanza kusini mwa jangwa
la sahara ambapo ujenzi na uendeshaji wa huduma hii ya reli
unatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya China.
Picha zote ni kutoka BBC.

Treni
hizi za umeme zitakua na uwezo wa kuhudumia Abiria elfu kumi na tano
ndani ya dakika 60 ambapo Treni moja inaweza kubeba abiria 286 kwa
wakati mmoja.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment