
Mwanamke wa Misri anayeaminiwa kuwa
mwenye uzito wa juu zaidi duniani akiwa na kilo 500, amefanyiwa
upasuaji wa kupunguza unene chini India.
Msemaji wa hospitali ya
Saifee mjini Mumbai amesema kuwa Eman Ahmed Abd El Aty, mwenye umri wa
miaka 36, amepungua kilo 100 baada ya upasuaji.
" Tunajaribu
kumuwezesha kuwa mwenye nguvu za mwili kuweza kusafiri nyumbani Misri
haraka iwezekanavyo," ilieleza taarifa ya hospitali.
Familia yake
ilisema kuwa hajawahi kuondoka nyumbani kwao kwa miaka 25 hadi siku
aliposafirishwa hadi India mwezi Januari kwa ndege.
No comments:
Post a Comment