Tuesday, August 2, 2016

JIKINGE NA MAUMIVU YA KIFUA (KICHOMI)

MAUMIVU YA KIFUA (ANGINA PECTORIS)

Maumivu haya zaidi uhusisha moyo na yanapomtokea mtu huchukua muda mfupi na huisha, aina hii ya maumivu kwa lugha nyingine ya kitaalamu huitwa Kilio cha moyo ambapo misuli ya moyo inayowezesha moyo usukume damu inakosa hewa ya oksijeni hivyo inachoka na kufanya kazi kwa kujilazimisha ndiyo maana hali ikizidi kuwa mbaya utajikunja inakulazimu upumzike au ukae chini.
Chanzo cha tatizo

Maumivu haya ya kifua kama tulivyoona hutokana na misuli ya moyo kufanya kazi huku ikikosa hewa ya oksijeni. Kwenye misuli ya moyo kuna  mishipa ya damu inayosambaza damu katika misuli hiyo.

Mishipa hiyo inayoitwa Coronary Artery. Mishipa hii ni midogo kwa hiyo huwa inaziba kutokana na mafuta mengi kuzunguka kwenye damu au ‘Cholesterol’ au kwa Kiswahili ‘lehemu.’ Mafuta haya huganda  ndani ya mishipa ya damu hivyo hupunguza kipenyo cha mshipa wa damu au bomba la kupitisha damu na mwishowe kuziba kabisa. Mishipa hii ikiziba katika upande mmoja wa moyo husababisha upande huo kitofanya kazi vizuri.

Mahitaji ya mzunguko wa oksijeni katika misuli ya moyo huwa makubwa pale unapojishughulisha kwa mazoezi, aidha kukimbia, kutembea harakaharaka au kupanda ngazi au mlima, hapo utajisikia pumzi inapungua na kifua kinauma.
Maumivu ya kifua zaidi huwa upande wa kushoto na wakati mwingine yakielekea mgongoni upande huohuo.

Jinsi tatizo linavyotokea
Kama tulivyoelezea jinsi maumivu yanavyotokea, mgonjwa atagundua kwamba anatatizo hili la Angina endapo siku zote anaishi vizuri tu, hana presha ya kupanda wala kushuka lakini si mtu wa kufanya mazoezi lakini akijishughulisha kwa mazoezi au kupanda ngazi anapata shida hasa kupanda mlima.

Maumivu anayoyapata katika upande huo wa kifua huwa kama vichomi ambapo kitaalamu tunasema ‘constricting, squeezing or choking’ anajihisi kama  ametiwishwa zigo zito kifuani kwake lakini akikaa na kupumzika  yanaacha.

Maumivu haya yana tabia ya kusambaa endapo yatakuwa makali au utakuwa unayavumilia, husambaa upande wa kifua kushoto kuelekea mgongoni na katikati ya kifua na kuhisi kama unakiungulia yaani moto mkali ndani ya kifua.

Mgonjwa pia anaweza kuhisi maumivu katika bega la kushoto au mabega yote.

Kwahiyo hata ukiwa umekaa tu utahisi mabega yanauma na kifua kinauma katikati na kusambaa hadi mgongoni na mwili kuwa mchovu. Hali ikiwa mbaya maumivu husambaa hadi shingoni na kwenye mataya na kujihisi kila wakati wewe ni mgonjwa na kuhangaika mara upime malaria, Typhoid au uende kwenye masaji.

Hali hii ya uchovu wa mwili na kujihisi mgonjwa kila wakati husababishwa na misuli ya moyo kutopata oksijeni ya kutosha na mara myingi vipimo vingi utakavyofanyiwa utaambiwa huna tatizo lakini wewe bado unaumwa.

Hali hii huongezeka au huendelea hivyo siku hadi siku endapo akili yako itakuwa na msongo wa mawazo.

Maumivu ya kifua na mwili wakati mwingne huwa makali baada ya tendo la  ndoa.
Maumivu makali na uchovu hupungua dakika ishirini baada ya kujitokeza, unatakiwa upate muda wa kupunguza na  kama ulikuwa unafanya mazoezi uache hadi uonane na daktari wako wa uchunguzi na ushauri.

Uchunguzi
Utafanyika katika hospitali za mikoa, vipimo mbalimbali vinavyohusu moyo hufanyika, historia ya tatizo itachukuliwa kwa undani. Chunguza ulaji na unywaji wako na maisha unayoishi.

Athari za tatizo
Tatizo hili linaweza kukusababishia matatizo makubwa ya moyo ambapo upande mmoja wa moyo unaweza kufa au ‘myocardial infaretion’ endapo tatizo litaendelea kwa muda mrefu, vilevile unaweza kukutwa na mauti ghafla kwa shinikizo au mshtuko wa moyo.
‘Heart Attack. Magonjwa haya tutakuja kuyaona hapo baadaye. Tatizo huathiri nguvu za kiume na  kukosesha hamu ya tendo la ndoa.

Ushauri
Endapo unafanya mazoezi halafu unashindwa kutokana na dalili tulizozielezea au unatembea kwa kupandisha kilima au ngazi inakuwa tabu, basi usidharau muone haraka daktari wako kwa uchunguzi. Pia hata ukiona kabla na wakati wa tendo la ndoa unahisi moyo unaenda mbio basi wahi hospitali. Epuka unywaji pombe, ulaji wa vyakula vyenye mafuta na uvutaji wa sigara,
Pendelea kufanya mazoezi, Tatizo ni kubwa  kwa wasiofanya mazoezi, tumia hata nusu saa kwa siku.
MG BLOG

ALALA UWANJA WA NDEGE SIKU 10 KUMSUBIRI MKEWE

Asubiri mpenziwe siku 10 katika uwanja wa ndege

Je penzi la kweli lipo ?
Hilo ndilo swali linaloulizwa sana katika mitandao nchini China.
Hii ni baada ya raia mmoja kutoka Uholanzi kusafiri maelfu ya kilomita ili kukutana na mpenziwe raia wa uchina ambaye walikutana kwenye mitandao ya kijamii.
Hata hivyo mpenziwe hakujitokeza hata baada ya kusubiri katika uwanja wa ndege kwa siku 10!
Amini usiamini alimsubiri kwa siku 10!
Alexander Pieter Cirk, 41, alifunga safari hadi jimbo la Hunan kukutana na mpenziwe mwanamke kutoka Uchina ambaye anafahamika kwa jina Zhang.
Na baada ya kumsubiri kwa siku kumi katika uwanja wa ndege wa Changsha hakujitokeza ,,Cirk alienda kufanya subira na mwishowe akalazimika kulazwa hospitalini kwa uchovu wa mwili na roho.
Cirk ameviambia vyombo vya habari kuwa walikutana na bi Zhang mwenye umri wa miaka 26 miezi miwili iliyopita na penzi lao likachipuka.
Hata hivyo alipofika China akagundua kuwa wanawake wengi nchini humo wanafanana, na akashindwa kumpata Zhang kwa simu.
Ripoti hiyo ilipopeperushwa kwenye runinga ya taifa , bi Zhang alijitokeza na kuwaamnbia Wachina kuwa alidhania kuwa ni utani tu kama vile maisha ya mjini kwa wanawake wengi ambao huambiwa kuwa wanapendwa.
''Ni kweli kuwa tulikuwa tunapendana lakini nilianza kumshuku huenda alikuwa ananichezea shere''
Alinitumia picha za tiketi ya ndege na hakunipigia simu baada ya hapo''
Kwa hivyo nikapuuza nikijua kuwa ni mzaha tu''bi Zhang aliiambia Hunan TV.
Zhang alisema kuwa ule wakati alipokuwa akimtarajia ,yeye alikuwa amefanyiwa upasuaji katika mji mwengine wa mbali.
Hangeweza kumpokea katika uwanja wa ndege.
katika mitandao ya kijamii tukio hilo limewaacha wengi wasijue iwapo ilikuwa ni penzi la kweli ama ni ujinga wa kuzaliwa.

BOMBA LA MAFUTA UGANDA HADI TANGA LAPATIWA JINA

Bomba la mafuta litakalojengwa kutoka Uganda mpaka Tanga lapatiwa jina hili

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo April 24 2016 aliwasili Tanzania akitokea Uganda alipokwenda kwenye mkutano wa majadiliano ya bomba la mafuta lipite wapi kati ya Tanzania au Kenya na bandari ya Tanga ikafanikiwa kupita na kukubaliwa kuwa bomba la mafuta hilo litaelekea bandari ya Tanga.
Hivi karibuni viongozi wa Tanzania na Uganda walikutana na kujadili bomba hilo litaitwaje kwa ajili ya kufahamika zaidi na Waziri wa nishati na madini, Sospeter Muhongo alihudhuria kikao hicho, hapa amebainisha jina la bomba hilo………..
>>>’ni la nchi mbili la Uganda na Tanzania kwenye kikao chetu kule Uganda tulilipatia jina linaitwa ‘The East African crude oil high plant’ ndio jina lake
millardayo

HADITHI ,MWANAMKE SEHEMU YA 51

SIMULIZI ZA FAKI A FAKI 0713 340572

MWANAMKE 51

ILIPOISHIA

Tukatoka tena. Tulijipakia kwenye gari tukaondoka.

Breki ya kwanza ilikuwa mbele ya hoteli moja iliyokuwa katika mtaa mwingine. Ilikuwa hoteli ndogo ya ghorofa moja, Ilikuwa imeandikwa kwa herufi kubwa. AL ASAD.

“Hii ndio hoteli ambayo nitakuachia wewe, itakuwa kama mali yako kwani tutakuwa tunagawana faida kila mwezi na kila mwaka kama utapenda kuendelea kubaki Somalia” Abdi aliniambia tukiwa bado tupo kwenye gari.

Alipoona nilikuwa nikiiangalia angalia ile hoteli, aliniambia.

“Tushuke uione vizuri”

Tukashuka.

Tuliingia ndani ya ile hoteli. Kwa kweli ilikuwa imechangamka.

“Sasa nani anaiendesha kwa hivi sasa?” nikamuuliza.

“Yuko mtu lakini nitamuondoa”

“Sasa ni kwanini umuondoe?”

“Lengo langu ni kukunufaisha wewe rafiki yangu au nimefanya kosa?’

“Hapana. Ni vizuri”

Abdi alinitembeza hoteli nzima kisha tukaingia katika ofisi ya meneja.

Meneja mwenyewe alikuwa mtu mzima. Kichwa chake kilishaanza kutoka mvi.

SASA ENDELEA

Walizungumza kwa kisomali huku meneja huyo akinikodolea macho.

Walizungumza kwa karibu robo saa kisha tukatoka.

“Yule ndiye meneja aliyeko sasa” Abdi aliniambia wakati tunatoka nje ya hoteli hiyo.

“Utamuhamishia mahali pengine au unammuondoa kabisa?’ nikamuuliza.

“Nitamfikiria”

“Umeshamwambia?”

“Nilitaka kwanza nikubaliane na wewe”

“Mimi nimeshakubali”

“Una uzoevu wa kuendesha hoteli?”

“Kwa kweli sina uzoefu huo”

“Utajifundisha hapa hapa. Ninaamini hutaweza kushindwa”

“Nitajaribu”

“Kazi yako itakuwa kuongoza na kukagua. Kuna kijana ambaye amesomea uendeshaji wa hoteli yuko pale atakusaidia”

“Nafikiri nitaweza. Usiwe na wasiwasi”

Baada ya hapo hatukuzungumza tena. Mwenzngu alikuwa amenyamaza, sikujua alikuwa akiwaza nini. Mimi nilikuwa na mawazo ya kubaki Somalia kuendesha shughuli ya hoteli.

Kikubwa kilichonipa tamaa ni kuwa kazi ya umeneja wa hoteli ni ya heshima na aliniambia kuwa angenipa ile nyumba pamoja na gari. Isitoshe tungegawana mapato ya hoteli..

Nilijiambia kama ningeweza kuchuma pesa pale Somalia na kurudi kwetu nikiwa na utajiri kama alivyoniahidi Abdi, sikuona haja ya kung’ang’ania kurudi Tanga ambako sikuwa na hakika kama nisingefukuzwa kazi kutokana na kutoonekana kazini kwa kipindi kirefu bila taarifa yoyote.

Abdi akanipeleka nyumbani kwake. Ilikuwa nyumba nzuri ya ghorofa moja iliyokuwa ndani ya geti. Mlinzi wake alitufungulia geti. Gari la abdi likaingia.

Kulikuwa na banda la magari lakini Abdi alilisimamisha gari hilo mbele ya mlango wa nyumba yake ya kifahari.

Tukashuka. Abdi alikwenda kufungua mlango akaniambia.

“Karibu kaka”

Tukaingia ndani. Alikuwa na sebule ya kupendeza iliyokuwa imepambwa vizuri kwa fanicha za thamani. Wakati tunaingia kulikuwa na msichana mmoja aliyekuwa akifanya usafi kwa kutumia kufaa maalum cha kuondoa vumbi.

“Karibu ukae” Abdi aliniambia huku naye akikaa. Akaongeza.

“Jisikie uko nyumbani. Hapa ndio kwetu bwana”

Nikawa natupa macho huku na huko kuiangalia sebule.

“Asante. Nimefurahi kupafahamu nyumbani kwako”

“Utakunywa kahawa?” Abdi akaniuliza.

“Hapana”

“Tangu uje Somalia sijakuonesha nyumbani kwangu. Hii nyumba ni yangu na mimi ninaishi hapa” Abdi aliendelea kuniambia kisha akaongeza.

“Unaweza kuona nyumba iko kimya kwa sababu watoto hawapo”

“Wako wapi?”

“Shemmeji yako amekwenda kwao Kismayuu. Mama yake ni mgonjwa. Atarudi pindi mama yake akipata nafuu”

Yule msichana aliyekuwa akifanya usafi alikuwa ameshaondoka.

“Nilipomuona huyu msichana nilidhani ndiye shemeji?”

“Hapana. Yule ni mfanyakazi wangu. Kwa sasa ninaishi na wafanyakazi wangu tu”

Hatukukaa sana hapo. Abdi akainuka na kuniambia.

“Sasa acha nikurudishe kule hoteli. Nataka niende shambani kwangu. Niliambiwa baadhi ya ng’ombe wangu ni wagonjwa”

Tukatoka na kujipakia tena kwenye gari, tukaondoka.

Abdi alinirudisha hotelini akaniacha na kuondoka. Niliingia chumbani nikaketi. Mawazo ya Zena yakaanza kunijia. Sikutaka kuendelea kumuwaza mwanamke huyo wa kijini lakini mawazo yake yalinijia kwa nguvu na sikuweza kuyazuia.

Kikubwa kilichosababisha nimuwaze ni kule kujitokeza nyumbani kwa yule mzee wa kisomali na kumpiga kibao yule mzee. Mpaka muda ule tukio lile lilikuwa kama kitendawili nilichoshindwa kukitegua.

Lakini jambo moja ambalo halikuwa na shaka akilini mwangu ni kwamba Abdi na yule mzee wa kisomali walikuwa wanajua ni kwanini Zena alitokea pale.

Kama walikuwa hawajui ni lazima Abdi angeonesha mshangao wake na angenieleza kitu. Lakini hakutaka kunieleza chochote kama vile ilikuwa ni siri.

Kadhalika sikuweza kujua yule mzee alikuwa ni nani, ana uhusiano gani na Abdi na kwanini nilimuota usiku akiniingiza ndani ya kaburi?

Pia nilijiuliza kile walichokuwa wanasoma pale ni kitu gani na kwanini kuliwekwa vitu mbalimbali kama vya uganga? Kwa kweli licha ya kujiuliza mara kadhaa sikupata jibu la kuridhisha.

Kwa vile sikuweza kuelewa kitu niliona nisiumize kichwa kwa kujiuliza maswali ambayo hayakuwa na majibu. Nikayaacha mawazo yale.

Siku ile sikumuona tena Abdi hadi siku ya pili yake ambapo alikuja hoteli asubuhi kunijulia hali.

“Nyumba yako itawekewa fanicha mpya leo. Kesho utaanza kuishi kule na kesho kutwa utakwenda kuanza kazi kule hotelini. Yule meneja ataondoka leo” Abdi akaniambia.

“Sawa”

“Amour unajua kuendesha?”

“Kuendesha nini?”

“Nina maana kuendesha gari”

“Ninajua lakini sikuja na leseni yangu”

“Si tatizo. Tutakwenda studio utapiga picha kadhaa za  paspoti, baadhi yake tutazitumia kukutengezea leseni ya hapa Somalia”

“Nitaipata lini hiyo leseni?’

“Kesho tu utaweza kuipata”

“Bila mimi mwenyewe kwenda kujaribiwa?”

“Hiyo kazi niachie mimi. Hata paspoti utapata bila kwenda wewe mwenyewe”

“Lakini hiyo paspoti itakuwa ya nchi gani?”

“Wewe ulitaka ya nchi gani?”

“Ya Tanzania”

“Utaipata bila shaka yoyote. Hapa kuna mabingwa wa kugushi. Nipe wiki moja tu. Utawekewa na mihuri ya tarehe uliyoingilia hapa Somalia”

Aliponiambia hivyo nilitabasamu.

“Inaonekana wewe hushindwi na kitu hapa Somalia” nikamwambia.

“Serikali yenyewe nimeiweka mikononi mwangu. Kuna maafisa wa polisi ambao wanakuja kuchukua mishahara kwangu kila mwezi kwa ajili ya kulinda miradi yangu. Wewe umeona mwenyewe juzi meno ya tembo tulivyoyaingiza na kuyapakia kwenye meli. Usifikiri kuwa polisi hawajui, wanajua. Baadhi ya mawaziri pia ni marafiki zangu. Likitokea tatizo niwapigia simu”

“Ninakuamini. Mambo yako ni makubwa!”

Nilipomsifu Abdi alicheka akanipa mkono. Alionekana kuwa ni mpenda sifa.

Tuliondoka hapo Hoteli tukaenda studio kupiga picha za papo kwa papo. Alichukua picha zangu kadhaa za usawa wa paspoti.

Wakati ananirudisha hotelini, nilimwambia kuwa nilikuwa ninahitaji saa.

“Saa tu, twende dukani tukanunue” akaniambia.

NAAM. MAMBO YANAZIDI KUPAMBA MOTO!

TUKUTANE TENA KESHO

KUELEKEA UCHAGUZI , MAREKANI

Trump asema Hillary Clinton ni 'shetani'

Mgombea wa chama cha Republican nchini marekani Donald Trump amemtaja mshindani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton kuwa 'shetani'.
Akizungumza kwenye mkutano huko Pennsylvania  Trump alimshambulia Bernie Sanders kwa kumuachia nafasi Bi Clinton.
Tajiri huyo alisema kuwa Sanders alifanya makubaliano na 'shetani' .
Wanachama wa Democrat na Republican wememkosoa bwana Trump kutokana na matamshi yake kuhusu wazazi wa mwanajeshi M'marekani muislamu aliyeuawa vitani nchini Iraq.

SOMA KURASA ZA MAGAZETI MWANZO MWISHO NA NEW AGE EDUCATION CENTRE TANGA 0717 713866

New Age Education Centre Tanga mabingwa wa kufaulisha wanafunzi Tanga walioko Mkabala na TANESCO  hakikutaka kurasa za Magazeti ya kupite, kwa jitihada za kituo hicho wamekusogezea mbele yako. 

Monday, August 1, 2016

EPUKA MAUMIVU YA KICHWA , JIBU LIKO HAPA

KAMA UNASUMBULIWA NA MAUMIVU YA KICHWA SOMA HAPA

Maumivu ya kichwa ni hali inayosumbua watu wengi kwa sasa, hii ni kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ambayo yanakuja na dalili za kichwa kuuma, uchovu wa kila siku, hewa nzito ya carbon dioxide na kelele nyingi za viwandani na magari.

Baadhi ya magonjwa na tabia zinayosababisha kichwa kuuma ni kama zifuatazo.

1. Utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe.
 2. Magonjwa ya macho mfano  refractive errors
 3. Magonjwa ya ubongo mfano i.e meningitis
 4. Uvimbe ndani ya ubongo i.e brain tumour
 5. Magonjwa ya mifupa ya usoni i.e sinusitis
 6. Cervical degenerative osteoporosis i.e magonjwa ya mifupa ya uti wa mgongo
 7. Magonjwa ya moyo i.e presha ya damu
 8. Mgandamizo wa mawazo.
Matibabu ya kiasili
Kutibu chanzo yaani ugonjwa uliosababisha kichwa kuuma ndio njia bora ya kutibu maumivu ya kichwa.

Kama chanzo cha maumivu ya kichwa hayafahamiki njia zifuatazo zinaweza kutibu dalili na kupunguza maumivu hayo.


  • Kukandwa na kutomaswa na maji ya moto nyuma ya shingo.{ hot compresses and massages.}
  • Kula chakula kisicho na nyama na chenye chumvi kidogo sana.{ vegetarian diet}
  • Weka kitambaa cha maji ya uvuguvugu kwenye paji la uso kuongeza mzunguko wa damu.
  • Tembea sehemu yenye uwazi mkubwa na hewa ya kutosha.
  • Fanya mazoezi ya kuogelea.
  • Ungea na daktari au mwanasaikolojia ambaye anaweza kuatambua ugonjwa wa akili ambao unasababisha maumivu hayo.
  • Pata mda mrefu wa kupumzika na kupata usingizi wa kutosha.


Matibabu ya dawa za kisasa.
Unaweza kutumia dawa ya maumivu kama diclofenac, paracetamol, ibuprofen na kadhalika pale maumivu yanapokua makali sana.bonyeza haya maneno ya kijani kusoma zaidi.
MG BLOG

JITIMU MAGONJWA KWA KUNYWA MAJI YA VUGUVUGU

IITIBU MAGONJWA MBALIMBALI KWA KUNYWA MAJI YA UVUGUVUGU

Ifuatayo  ni  orodha  ya  baadhi  ya  magonjwa  yanayo weza  kutibiwa  kwa  maji  ya  Uvuguvugu

- pumu= asthma

- shinikizo la damu= hbp

- migraine / kichwa= migraine/ headache

- ugonjwa wa sukari= diabetes

- upungufu wa damu= anemia

- maumivu nyuma= back pain

- mawe katika figo= urinary calculus

- maambukizo wa haja ndogo= urinary tract infection

- cholesterol= cholesterol

- baridi yabisi & ugonjwa wa mifupa= rheumatism & arthritis

- kiharusi =stroke

- udhaifu wa mwili =sexual and body weakness

- kuchoka & uchovu = tiredness & fatigue

- tonsili =tonsillitis

- vijidudu vya tumbo = gastroenteritis (stomach virus)

- mafua/homa =colds, flu & fever

- kukosa usingizi= insomnia (lack of sleep)

- kichome kwenye roho= heartburn

- kidonda tumboni =stomach ulcer

- kuvimbiwa (ugumu kupata haja kubwa) =constipation

- kutetemeka mwili kutokana na umri= parkinsonism

- kupoteza nywele (upaa) =hair loss (baldness)

- magonjwa ya ngozi=skin diseases (psoriasis)

- kasoro ya ubongo =alzheimer (defects of the brain)

- maradhi ya moyo =heart disease

- saratani= cancer

- usafisha hedhi ya kila mwezi ya wanawake= purifying women's monthly period

MATUMIZI:
Kunywa    glasi  mbili  ya  maji  ya Uvugvugu  asubuhi  unapo amka kabla ya kwenda chooni kupiga mswaki na kabla  ya  kula  chochote  na unapo maliza kupiga mswaki kunywa tena

Maji ya Uvuguvugu glasi 1 na kaa kwa muda wa saa 1 ndio waweza kula chakula cha asubuhi. Na wakati wa mchana kunywa tena glasi 2 kabla ya kula kitu kisha kaa baada ya saa 1 kupita waweza kula chakula cha mchana. Na wakati wa   usiku kabla ya kula chakula

cha usiku kunywa tena Maji ya Uvuguvugu glasi 2 kaa baada ya saa 1 kupita waweza  kula. kabla  ya  kulala kunywa glasi 1 ya Maji ya Uvugvugu kisha waweza kulala. Fanya  hivyo kila siku  katika maisha yako maradhi yote yatakuondokea kabisa utapona.
MG BLOG

EPUKA KUNYWA POMBE WAKATI WA UJAUZITO

YAFAHAMU MADHARA YA KUNYWA POMBE KIPINDI CHA UJAUZITO

Kipindi cha ujauzito kwa mama ni kipindi muhimu sana ambacho kwa wakati huu mama hatakiwi atumie kitu chochote cha kujitibu bila ushauri wa daktari kwani kinaweza kudhuru mtoto lakini pia kipindi cha ujauzito ni kipindi ambacho mama hatakiwi kunywa kileo chochote kile unachokifahamu.

Sio bia, sio spirit, wala mvinyo au wine. wanawake wengi wa siku hizi hubeba mimba bila kufahamu kwamba wana mimba na huja kugundua baada ya mwezi mmoja au miwili baada ya kumshindilia mtoto pombe za kutosha.tabia hii ina madhara makubwa sana kwa mama na mtoto kama ifuatavyo...

1. Mtoto kua na umbo la ajabu; mtoto huweza kuzaliwa na kichwa kidogo, uso kama bapa na macho madogo sana. dalili hizi huweza kuanza kuonekana katika umri wa miaka 2 na mara nyingi mtoto hua tofauti na wenzake.

2. Kuchelewa kukua; pombe huingilia mfumo wa ukuaji na kumchelewesha mtoto kufanya baadhi ya mambo kama kutambaa, kutembea, kuongea na kadhalika. ukimuangalia mtoto mwenye umri kama huo huo ataonekana mkubwa kuliko huyu anayetumia pombe.

3. Kushindwa kujifunza; mara nyingi watoto hawa hua wabovu sana darasani na kushindwa kuelewa vitu kama watoto wengine..mata nyingi mzazi huishia kulalamika na kumshangaa mtoto na kumuona mzembe bila kujua chanzo ni yeye...

4. Kuchelewa kula kwa mtoto; kawaida mtoto anatakiwa anywe maziwa tu kwa muda wa miezi sita, tena maziwa ya mama baada ya hapo aanze kula chakula. mtoto aliyepata madhara ya pombe hushindwa kunyonya na kuchukua muda mrefu sana kuanza kula.

5. Matatizo ya viungo; siku hizi kuna picha zinatumwa sana mitandaoni zikionyesha mtoto kazaliwa bila mikono, miguu au kaunganikana kichwa na pacha mwenzake. hizo sio bahati mbaya kama watu wanavyodhani ila hayo ni madhara ya vitu ikiwemo pombe.

6. Kuharibika kwa ujauzito; pombe inaweza kuingilia mfumo wa homoni za mwanamke au kufungua mlango wa uzazi na kusababisha kuharibika kwa mimba, mimba huweza kuharibika ghafla au taratibu kulingana na aina ya pombe.

7. Kuzaa kabla ya muda; kwenye mimba kubwa pombe inaweza kusababisha kuanza kwa uchungu kabla ya muda na kumzaa mtoto ambaye hajakomaa maarufu kama kabichi.

Mwisho; hakuna kipindi ambacho ni salama kunywa pombe kipindi cha ujauzito, kama hauhitaji mtoto kwa sasa tumia vizuizi vya mimba lakini kama unakunywa pombe na kufanya ngono bila kinga utajikuta una mimba ambayo imeshaathirika na pombe tayari na ukipata mimba acha pombe kabisa.
MG BLOG

WANASHERIA TANGA WAPIGWA MSASA KUSIMAMIA MIKATABA NA UBIA SEKTA BINAFSI NA SERIKALI



 Washiriki wa Semina ya kujengewa uwezo kusimamia mikataba ya Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi wakifuatilia hutuba ya  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gerson Mdemu, wakati w aufunguzi wa warsha hiyo Leo ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.



 Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gerson Mdemu, akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Mkuu wa Mkoa mara baada ya kufungua Semina ya siku nne ya kuwajengea uwezo maofisa wa sheria wa Serikali namna bora ya kuendesha mikata na ubia kati ya Serikali na sekta binafsi nchini.
 Kamishna wa Sekta binafsi na Serikali, Dr, Frank Mhilu, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Semina ya siku nne ya kuwajengea uwezo maofisa wa Serikali na wanasheria namna bora ya kuendesha mikataba na ubia kati ya Serikali na sekta binafsi nchini.


Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gerson Mdemu, akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Mkuu wa Mkoa mara baada ya kufungua Semina ya siku nne ya kuwajengea uwezo maofisa wa sheria wa Serikali namna bora ya kuendesha mikata na ubia kati ya Serikali na sekta binafsi nchini.

MWIZI WA MITANDAONI AKAMATWA NIGERIA

Mlaghai mkubwa wa mtandaoni akamatwa Nigeria

Raia mmoja wa Nigeria aliyetuhumiwa kuanzisha ulaghai mkubwa wa mitandao, ambapo zaidi ya dola milioni sitini ziliibwa, amekamatwa katika mji wa Port Harcourt Kusini mwa nchi hiyo.

Kukamatwa kwake kulifaulu baada ya ushirikiano wa pamoja kutoka kwa Polisi wa kimataifa- Interpol na mamlaka kukabiliana na ufisadi nchini Nigeria.

Polisi wa kimataifa - Interpol, wanasema kuwa mtu huyo mwenye umri wa miaka 40 anayefahamika kama 'Mike', anaaminika kuhusika na ulaghai wa zaidi ya dola milioni 60 na ana matapeli wengi wanaofanya kazi katika mataifa mbalimbali duniani.

Mtandao wake mkubwa uko nchini China, bara Ulaya na Marekani na mojawepo ya ulaghai huo ni wa ulipaji fedha ambapo kampuni mbalimbali za kibiashara hulipa pesa katika akaunti inayoaminika ni halali, lakini kumbe akaunti hizo zinadhibitiwa na magenge hayo ya wahalifu.

ARSENAL YAFANYA KWELI MAREKANI

Arsenal yatakata Marekani, yaichapa Chivas 3-1

Klabu ya soka ya ligi kuu ya nchini Uingereza, Arsenal, imeichapa mabo 3-1, klabu ya Chivas, ya ligi kuu ya soka ya Mexico, kwenye mchezo wa kirafiki.

Arsenal imemaliza ziara yake ya nchini Marekani, kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chivas ya nchini Mexico, mjini, Los Angeles, Marekani, alfajiri ya leo.

Mlinzi mpya wa klabu hiyo, Rob Holding, aliifungia Arsenal bao la kwanza kwenye dakika ya 34, kabla ya Alex Oxlade-Chamberlain na Chuba Akpom kuongeza mabao ya kipindi cha pili.

Chivas ilipata bao la kufutia machozi kutoka kwa mchezaji aliyeingia kutoka benchi, Angel Zaldivar, akifunga kwa penati, mbele ya watazamaji 25,000 kwenye uwanja wa Stub Hub Center, unaomilikiwa na klabu ya L.A Galaxy.

KUMEKUCHA MAREKANI

Mshauri wa Trump azungumza picha za utupu za mkewe Trump

Baada ya jarida la New York Post  la Marekani kutumia picha za utupu za mke wa Mgombea  urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump katika jarida lao walilolitoa July 31 2016 ambalo limesababisha headlines mitandaoni.
Leo August 1 2016 Kituo kikubwa cha habari CNN kimempata kwenye exclusive interview mshauri mkuu wa mgombea huyo Jason Miller na ameyazungumza haya…..Picha hizo zina miaka 20 kipindi kabla Donald Trump na Melania kukutana na hatuna tatizo na jarida la New York Post kutumia picha za utupu za Melania Mwili wa binadamu ni sherehe ya sanaa, hakuna kitu cha kushangaza Melania ni mwanamke mzuri”
millrdayo

JAMII ILIYO NA WATOTO WALEMAVU YAASWA KUACHA TABIA YA KUWAFUNGIA NDANI



Tangakumekuchablog
Tanga, WAZAZI na Walezi wa watoto wenye ulemavu Tanga, wametakiwa kuacha kuwafungia ndani na badala yake kuwapeleka shule na kuweza kupata elimu ambayo itaweza kuwasaidia katika maisha yao mbeleni.
Akizungumza katika  ufunguzi wa mashindano ya kuibua vipaji vya kuchora na kutunga mashairi jana, Afisa Utamaduni jiji la Tanga, Rose Sempoli, alisema kuna baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakiwafungia ndani.
Alisema kitendo hicho kinawanyima haki ya kupata elimu ambayo itawasaidia katika maisha yao mbeleni hivyo kutakiwa kuacha tabia hiyo na kuwataka kuwapeleka katika vituo vya walemavu na kuwapeleka shule.
“Kuwa na ulemavu sio dhambi wala vibaya kwani ni maumbile ya kibinadamu ambapo mtu yoyote anaweza kuupata katika maisha yake, kwa pamoja tukomeshe vitendo vya ufungiaji wa watoto ndani” alisema Sempoli na kuongeza
“Jamii hii wako na vipaji wakati mwengine zaidi ya wengine hivyo kuwafungia ndani kwa ulemavu wao ni kuwakatili na kuwaharibia maisha yao ya mbeleni” alisema
Aliitaka  jamii kwa pamoja kushirikiana na kuwaibua watu wanaowafungia ndani watoto wenye ulemavu na kusema kuwa anaamini ziko familia ambazo zimewafungiia ndani watoto hao hivyo kutakiwa kuwaibua.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Watoto wenye Ulemavu kituo cha Watoto (YDPC) Mtindi Jonathan, alisema kituo hicho kiko na watoto wenye ulemavu vipaji lakini hawana watu ambao wanaweza kuwaendeleza.
Alisema kuna wachoraji wa michoro na watunga mashairi na insha lakini vipaji vyao vinaishia kituoni hivyo kuwataka watu wenye mapenzi mema na jamii hiyo kuwasaidia.
“Hapa kituoni tuko na watoto wenye vipaji tena nazweza kusema zaidi ya jamii nyengine, tumeona hapa wakichora michoro utadhani imechorwa na mashine, hii ni kuonyesha kuwa walemavu nao wako na mchango katika Taifa” alisema Jonathan
Alisema kama watoto hao watapatiwa misaada ya hali na mali wanaweza kuwa msaada kwa Serikali kwa kutoa watu wenye vipaji mbalimbali na kuweza kupunguza uhaba wa wataalamu wa fani mbalimbali.
                                            Mwisho


  Watoto wenye ulemavu wa  viungo, viziwi, ngozi na akili wakiwa katika foleni ya chai kabla ya kuingia ukumbini kuingia katika mashindano ya kutafuta vipaji fani mbalimbali ikiwemo ya kuchora michoro na Insha yaliyoandaliwa na kituo cha watoto wenye ulemavu wa viungo (YDPC)  cha Tanga





  Mwenyekiti wa baraza la watoto wenye ulemavu kituo cha watoto wenye ulamavu cha Tanga (YDPC), Mtindi Jonathan, (kushoto)  akimpa zawadi ya begi mshindi wa kwanza wa kutunga Insha, Enjo Kimaro (kulia) wakati wa mashindano ya kuibua watoto wenye ulamavu