Arsenal yatakata Marekani, yaichapa Chivas 3-1
Arsenal imemaliza ziara yake ya nchini Marekani, kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chivas ya nchini Mexico, mjini, Los Angeles, Marekani, alfajiri ya leo.
Mlinzi mpya wa klabu hiyo, Rob Holding, aliifungia Arsenal bao la kwanza kwenye dakika ya 34, kabla ya Alex Oxlade-Chamberlain na Chuba Akpom kuongeza mabao ya kipindi cha pili.
Chivas ilipata bao la kufutia machozi kutoka kwa mchezaji aliyeingia kutoka benchi, Angel Zaldivar, akifunga kwa penati, mbele ya watazamaji 25,000 kwenye uwanja wa Stub Hub Center, unaomilikiwa na klabu ya L.A Galaxy.
No comments:
Post a Comment