Monday, August 1, 2016

MWIZI WA MITANDAONI AKAMATWA NIGERIA

Mlaghai mkubwa wa mtandaoni akamatwa Nigeria

Raia mmoja wa Nigeria aliyetuhumiwa kuanzisha ulaghai mkubwa wa mitandao, ambapo zaidi ya dola milioni sitini ziliibwa, amekamatwa katika mji wa Port Harcourt Kusini mwa nchi hiyo.

Kukamatwa kwake kulifaulu baada ya ushirikiano wa pamoja kutoka kwa Polisi wa kimataifa- Interpol na mamlaka kukabiliana na ufisadi nchini Nigeria.

Polisi wa kimataifa - Interpol, wanasema kuwa mtu huyo mwenye umri wa miaka 40 anayefahamika kama 'Mike', anaaminika kuhusika na ulaghai wa zaidi ya dola milioni 60 na ana matapeli wengi wanaofanya kazi katika mataifa mbalimbali duniani.

Mtandao wake mkubwa uko nchini China, bara Ulaya na Marekani na mojawepo ya ulaghai huo ni wa ulipaji fedha ambapo kampuni mbalimbali za kibiashara hulipa pesa katika akaunti inayoaminika ni halali, lakini kumbe akaunti hizo zinadhibitiwa na magenge hayo ya wahalifu.

No comments:

Post a Comment