Mgomo wa Madereva hatimaye umepata muafaka
Baadhi
ya Madereva na Makondakta wa Mabasi wanaondelea na Mgomo, wakiwa
wamekaa juu ya Kontena zilizopo kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Ubungo
jijini Dar es salaam kusubiria mustakabali wao, huku ulinzi Mkali wa
Jeshi la Polisi ukiwa umetawala eneo hilo.
Ghafla
likazuka tukio la kurushwa mawe kutoka kwa watu wasiojulikana waliokuwa
nje ya Stendi hiyo na kupelekea watu wote waliokuwa kwenye eneo hilo
kukusanyika sehemu moja ili kujinusuru.
Hali
ilikuwa tete pale mawe yalipokuwa yakirushwa, na kupelekea baadhi ya
viongozi pamoja na wanahabari waliokuwepo kwenye eneo hilo kukusanyika
sehemu moja. hivyo polisi walilazimika kutumia mbinu zao na kufanikiwa
kulituliza tukio hilo.
Baadhi ya wanahabari wakinawa maji kufuatia moshi wa Mabomu ya Machoni yaliyokuwa yakipigwa Ubungo mchana wa leo.
Ulinzi ulitawala eneo lote la Ubungo leo.
Baadhi
ya Madereva na Makondakwa wao wakimzogoa mmoja wa Viongozi wao
alikubali kuzungumza na Viongozi wa Serikali waliofika eneo hilo.
Muda
mfupi baadae, Aliwasili Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa
CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe ambaye alipokelewa kwa shangwe na Madereva
hao.
Shangwe zikiendelea.
Mmoja wa viongozi wa Madereva akiwasihi wenzake kutulia ili kuwasikiliza viongozi waliokwenda kuwasiliza.
No comments:
Post a Comment