Kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano haya dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.
Maandamano haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.
Aidha wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na Serikali ya kutaka kutanzua mzozo ulioko wa kisiasa.
Uamuzi ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki kadhaa.
Tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa jirani.
No comments:
Post a Comment