Liverpool:Sterling apata mtetezi
Nyota wa Liverpool Raheem Sterling ametetewa kwa kuwa na hamu kujiunga na vilabu vikubwa.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool huenda asilaumiwe kwa kuonyesha hamu ya kung'aa zaidi na kutaka kushinda vikombe.Hii ni kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Blackburn,Chris Sutton.
Tangu alipoanza kuonyesha nia yake yeye na wakala wake waliandamwa na kupingwa na wacheazaji wa zamani wa Liverpool.
"Sidhani kwamba uamuzi wake unahusu fedha" alisema Sutton
''Nahisi Sterling "anachotaka tu ni kujiunga na timu kubwa".
No comments:
Post a Comment