Mkenya kwenye headlines za kunyongwa China! safari yake ilikua Nairobi – China.
Afisi ya ubalozi wa kenya nchini Uchina
umethibitisha kwamba huenda Floviance akanyongwa mwaka huu baada ya
kifungo chake cha miaka miwili kukamilika na haya maneno ni kwa mujibu
wa dada yake ambaye ni Judith Owino.
Judith anasema hakufahamu kuwa dada yake
alikuwa amesafiri kwenda China hadi alipopata habari kutoka
ubalozi wa kenya nchini humo.
Serikali ya uchina hata hivyo ilimwarifu
Judith kwamba alikuwa na muda mfupi kugeuza hukumu hiyo na kuzuia dada
yake asinyongwe, walinishauri nitafute wakili hivyo kwa sasa nahitaji
visa kwenda china maana mda unazidi kupotea.
Mpaka sasa Judith hajapata fursa ya
kuzungumza na Floviance kwani serikali ya china haikukubali hilo
lifanyike >>> ‘nilitamani sana kuongea nae lakini
walinikatalia, Floviane ana mtoto wa miaka minne aliyemuacha Kenya baada
ya kusafiri kwenda China’
No comments:
Post a Comment