Boresheni hali ya wafanyakazi :Amnesty
Shirika
la Haki za binadamu la Amnesty International ,linasema Qatar
inalazimika kuboresha hali ya wafanyakazi wahamiaji wakati huu nchi hiyo
inapoendelea na maandalizi ya Kombe la Dunia mwaka 2022.
Amnesty
wanasema Qatar imepiga hatua kidogo sana kutekeleza ahadi nyingi
walizozitoa mwaka jana, kwani wafanyakazi bado wanahitaji ruhusa kutoka
kwa waajiri wao ,kubadili ajira au kuondoka nchini humo,mabadiliko ya
malipo kwa wafanyakazi yanafanyika taratibu mno wakati ni jambo la
muhimu mno.Hata hivyo Serikali ya Qatar inasema mabadiliko makubwa yanakuja ifikapo mwishoni mwa mwaka huu,japo kuwa Amnesty inaitaka FIFA , kuishinikiza Qatar kuongeza kasi katika kuleta mabadiliko.
No comments:
Post a Comment