Ripoti ya miezi 8 kuhusu ajali ya gari zinazotembea bila dereva..
Dunia imekuwa na mengi ambayo
yanahusiana na Teknolojia.. kila siku kuna story mpya, moja ya
zilizowahi kuchukua headlines mwaka 2014 ilikuwa ni ishu ya magari
ambayo yanajiendesha yenyewe bila dereva.
Google pamoja na makampuni mengine yaliamua kuweka nguvu kwenye ubunifu huu, mwezi September 2014 California
Marekani iliruhusu magari hayo yaendelee kutembezwa katika barabara za
kawaida ambazo zinatumiwa na magari mengine pamoja na watu.
Ripoti iliyotoka leo May 11 2015
inaonesha kuwa katika magari 50 ambayo yanatembea bila dereva
California, zimewahi kutokea ajali nne tu ambazo zinahusisha gari hizo..
japo Google wanasema ajali ambazo zilitokea ni ajali ndogo tu za
kawaida.
Ripoti hii ni kama inatia ushawishi wa
nchi nyingine kuvutiwa na huu ubunifu na kuanza kutumia aina hii ya
magari.. kingine kilichopo njiani ni hili lori ambalo nalo liko njiani
kuja, nalo linatembea bila dereva.
Ungana nami kila wakati na niweze kukusogereza kila kinachonifikia hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment