Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza. Wapo Tanga mkbala na Bank ya CRDB simi 0715 7727246
MWANANCHI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick
amesema mvua zinazoendelea kunyesha zimevuruga Jiji na kusababisha
uharibifu mkubwa wa miundombinu ambapo watu nane wamefariki mpaka sasa.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Jiji kwa sasa
haliko kwenye hali nzuri kutokana na barabara zaidi ya 20 kuaribika,
madaraja kadhaa na makaravati kusombwa na maji na kusababisha kukatika
kwa mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo.
“Nimewaagiza
viongozi wa manispaa kufanya kila linalowezekana kurudisha mawasiliano
katika maeneo ambayo madaraja yamevunjika ili shughuli ziendelee kama
kawaida huku tukijipanga kwa ajili ya kurekebisha maeneo mengine
yaliyoathiriwa”— Said Meck Sadick.
Baadhi ya maeneo ambayo yameathirika
zaidi kutokana na mvua hizo ni pamoja na Keko, Chang’ombe Maduka Mawili,
Yombo Vituka, Vingunguti, Africana, Msasani Bonde la Mpunga, Jangwani,
Manzese, Kigogo, Mburahati, Boko na Basihaya.
“Barabara
nyingi zimeharibika ingawa Wilaya ya Kinondoni imeonekana kuathirika
zaidi, lakini tumeruhusu ziendelee kutumika kupunguza msongamano, ila
tutazifunga tena endapo mvua zitaendelea kunyesha ili kuepukana na
madhara yanayoweza kujitokeza, endapo zitatumika zikiwa zimefurika maji”– Meck Sadick.
“Tumefunga
kwa muda shule ya Msingi Vingunguti baada ya kuona imezingirwa na maji,
hata hao wanafunzi wasingeweza kusoma, lakini maeneo mengine masomo
yanaendelea kama kawaida ingawa hali ya maudhurio inaonekana siyo nzuri
kutokana na hali ya hewa”—Said Meck Sadick.
JAMBO LEO
Watu wawili wamefariki katika ajali na wengine 11 kujeruhiwa kutokana na ajali iliyotokea maeneo ya Kihonda, Morogoro.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Leonard Paul amesema
gari hiyo iliyopata ajali ilikuwa ikisafirisha msiba kwenda Kagera kwa
ajili ya mazishi, ilipofika eneo hilo iligongana na Basi la Mvula
lililokuwa lililotokea Kigoma kwenda Dar.
Kamanda huyo amesema majeruhi
wamekimbizwa Hospitali kwa ajili ya matibabu, kwa sasa Jeshi la Polisi
linamshikilia dereva wa basi la Mvula kwa ajili ya upelelezi.
HABARI LEO
Hakimu mstaafu wa Mahakama ya Mkoa Arusha, Keenja Manase amepandishwa Mahakama kwa kosa la kughushi nyaraka za Serikali na nyaraka za Serikali na kujipatia Mil. 200.
Manase
alisomewa mashitaka hayo matatu mbele ya Mahakimu watatu tofauti,
akashindwa kutekeleza msharti ya dhamana kwa Hakimu mmoja, muda mfupi
baadae akapandishwa Mahakamani na kusomewa mashitaka mengine.
Shitaka la mwisho kusomewa ilikuwa kesi ya kughushi na kuandika nakala ya barua yenye mhuri wa Jiji la Arusha.
HABARI LEO
Kamati ya Bunge ya PAC imeagiza Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Mafutaa Mohamed kuondolewa Hotelinii ambako amekaa tangu alipoteuliwa ambapo wamedai anaiongezea gharama Serikali.
Kaimu Mwenyekiti wa PAC, Ismail Rage
amesema Mkuu huyo wa Wilaya ikifika May 31 itakuwa siku yake ya mwisho
kukaa Hotelini hapo, ambapo amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa kuangallia
namna ya kumalizia ujenzi wa nyumba ya DC huyo.
Mhasibu wa Mkoa alipohojiwa na Kamati
hiyo kuhusu gharama inayotumika kulipia Hoteli hiyo alijibu kwa
kigugumizi kwamba wanalipia Tshs. 80,000/- kwa siku kutoka kwenye mfuko
mwingine wa Wilaya hiyo.
Mkuu huyo wa Wilaya amekaa kwa miezi miwili Hotelini tangu alipoteuliwa kutokana na nyumba yake kutokamilika kujengwa.
NIPASHE
Jeshi la Polisi Ruvuma linasaka kundi la
watu wanaodaiwa kuwa majambazi ambao walivamia na kuwapora pesa na mali
zenye thamani ya Mil. 8 watu ambao walikuwa wakielekea msibani Songea
vijijini.
Kamanda wa Polisi Ruvuma, Mihayo Miskhela amesema
siku ya tukio Mei 7 kundi hilo la watu wakiwa na marungu na mapanga
waliweka magogo na mawe barabani na kuliteka basi lililokuwa
likisafirisha msiba huo na kuwapora vitu hivyo watu 22 waliokuwa
wakisafirisha msiba.
Kamanda huyo amesema kuwa kundi hilo la
watu tisa waliteka pia gari nyingine ikiwemo lori na gari ndogo pia na
kuwapora vitu mbalimbali.
Watu hao waliwakamata na kuwapekua watu
wote waliokuwa kwenye magari hayo huku wakiwa wamejifunga vitambaa
vyeusi usoni na kisha kutokomea kusikojulikana.
No comments:
Post a Comment