Tangakumekuchablog
Tanga,WAFANYABIASHARA
soko kuu la Mgandini Tanga, wameutaka uongozi wa soko kujenga miundombinu ya maji ili nyakati za mvua
kunyesha kuondokana na kero ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi na tope.
Wakizungumza na waandishi wa habari
sokoni hapo jana, wafanyabiashara hao walisema kipindi hiki cha mvua wamekuwa
wakifanya kazi katika mazingira magumu na wateja kukimbia.
Walisema kwa hali ilivyo sasa ni
vigumu kwa wateja kufika sokoni hapo kwani mazingira ni magumu ya kumshawishi
mteja kufika na kununua bidhaa baada ya eneo kubwa kujaa maji na kufanya tope.
“Mazingira ya soko kipindi hiki cha
mvua zinazoendelea kunyesha ni hatari----eneo kubwa la soko limejaa maji na
tope kwa kweli hii ni hatari” alisema Kassim Mvumo mfanfabiashara wa nyanya
“Kila mwaka huwa tunawambia viongozi
wetu kuwa soko hili halina miundombinu ya kupitisha maji----sasa wenyewe
wanajionea” alisema
Alisema soko ambalo limekuwa
likitegemewa na wakazi wengi jijini humo uongozi wa soko unatakiwa kuliweka
katika mazingira mazuri ili wateja kuepuka kulikimbia.
Akizungumzia kero hiyo, Mwenyekiti
wa soko hilo, Adam Tindikai, alisema kero hiyo wanaitambua na uongozi wa soko
unafanya jitihada na halmashauri ya jiji ili kuweza kuimaliza kero hiyo.
Alisema kwa sasa wako katika
jitihada ya kuondosha maji yaliyotuwaa katika tope pamoja na kuondosha takataka
ikiwa na pamoja na kuweka mazingira mazuri
ya soko hilo.
“Kweli tuko na changamoto nyingi
katika soko letu hasa vipindi vya mvua----ila tuko katika jitihada za kukabilia
na kero hasa nyakati za mvua ili kuwawezesha wateja wanaotumia soko hili kuacha
kulikimbia” alisema Tindikai
Amewataka wateja na wafanyabiashara kuwa
na uvumilivu kipindi hiki cha mvua wakati uongozi wa soko uko katika jitihada
kuhakikisha kero zinamalizwa kwa wakati.
No comments:
Post a Comment