Serikali ya Ivory Coast imekuja na sheria hii kwa wanawake wanaopenda urembo…
Wanawake
wengi duniani wanaamini moja ya vitu vinavyowaongezea mvuto wa ngozi
zao ni kutumia mafuta yanayobadilisha ngozi zao au kwa jina jingine
mafuta ya kujichubua ngozi.
Wengi
wamekuwa wakifanya hivyo na kukumbana na maradhi mengi ikiwemo kupata
kansa ya ngozi kwa sababu kitaalamu wanatumia kemikali ambazo
hazifai kwa matumizi ya ngozi ya binadamu.
Ivory Coast
imeingia kwenye Headlines baada ya Wizara ya afya ya nchini humo kupiga
marufuku uingizwaji, uuzaji na usambazaji wa bidhaa zozote zenye uwezo
wa kuchubua rangi ya ngozi ya binadamu .
Bidhaa nyingi za kijichubua rangi ya
ngozi zinauzwa katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika na sasa
Serikali imeweka sheria kali ya matumizi ya kemikali hizo ambazo kwa
miaka ya sasa hata wanaume wamekuwa wakitumia na kufanya idadi kuwa
kubwa.
Christian Doudouko
ambaye ni Afisa anayesimamia matumizi ya madawa nchini humo amesema
wanawake wengi wamekuwa wakipatwa na magonjwa ya ngozi yanayopelekea
saratani bila kujijua.
No comments:
Post a Comment