Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi sita na wanaojiendeleza kielimu. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 7727246
MTANZANIA
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Katavi imemuhukumu mwalimu mstaafu wa shule ya msingi Mpanda Ndogo , Rashid Ndogo mwenye miaka 65 kifungo cha maisha jela baada ya kumbala mjuu wake wa miaka mitano na kumuharibu vibaya sehemu zake za siri.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili za mashtaka na utetezi.
Awali katika kesi hiyo mwendesha
mashtaka alidai mahakamani kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba
mwaka jana majira ya saa 2 na nusu usiku nyumbani kwake katika kijiji
cha Majalila.
Siku hiyo mshatakiwa alidaiwa kumbaka
mjuu wake wakati amelala chumbani akiwa na mtoto wa mshtakiwa ambaye
alishugudia baba yake akitenda kosa hilo la kinyama.
Siku ya tukio mke wa mshatakiwa alimwaga
mume wake kuwa amekwenda kufunga zizi la mbuzi lililokuwa jirani na
nyumbani kwao na mumewe kutumia mwanya huo kuingia chumbani kwa mjuu
wake na kuanza kumbaka huku mwanaye akishuhudia.
Mshakiwa alikamatwa na majirani siku
hiyo na kupelekwa kituo cha Polisi ambapo alifunguliwa mashtaka huku
mjukuu wake akikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu.
MTANZANIA
Jeshi la Polisi Dar limebaini mabaki ya mwili wa mmiliki wa shule ya Mtakatifu Zion, Anna Mizinga aliyeuawa Desemba mwaka jana na kutupwa kwenye shimo la choo cha shule yake.
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova
alisema mabaki ya mwili huo yalibainika Juni mwaka huu na tayari watu
watatu wanashikiliwa na Polisi wakidaiwa kufanya unyama huo.
Akifafanua juu ya tukio hilo Kova
alisema Februari mwaka huu mtu mmoja alitoa taarifa polisi juu ya
kupotea kwa mmiliki huyo tangu Desemba mwaka jana saa 11 jioni na
hakuonekana tena.
Alisema mmiliki huyo alindoka nyumbani
kwake na gari dogo aina ya Verosa akiwa na mtu mmoja ambaye naye ni
miongoni mwa watuhumiwa wanaoshikiwa na jeshi hilo na abada ya taarifa
hiyo walifungua jalada la uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa
hao.
Alisema mtuhumiwa wa kwanza alikamatwa Uchira, Moshi na kuwataja wenzake.
“Katika
mahijiano mmoja alisema yeye na marehemu waliondoka hadi shuleni kwake
na walipofika walivamiwa na watu wapatao wanne na kuanza kupigwa, lakini
yeye alifanikiwa kutoroka na kujificha katika uzio wa shule, na
aliwaona watu hao wakiendelea kumpiga mama huyo na kisha kumtupa katika shimo la choo kisha kutokomea na gari lake kusikojulika” Kova.
Watuhumiwa hao wanaendele kuhojiwa ili
kupata undani wa tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kuwatafuta na kuwakamata
watuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo.
MTANZANIA
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amemaliza safari yake ya kusaka wadhamini katika Mikoa yote ya Tanzania na kujikusanyia zaidi ya wadhamini laki 8.
Lowassa alianza safari ya kusaka
wadhamini Juni 4 baada ya kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM na
jana amehitimisha safari yake hiyo katika Mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni za CCM,
kada anayewania kugombea Urais, anatakiwa kuwa na wanachama
waliomdhamini 450 kutoka Mikoa 15 ikiwemo mitatu kutoka Zanzibar.
Katika baadhi ya Mikoa ambayo Lowassa alipata wadhamini wengi ni pamoja na Dar es salaam, Arusha, Morogoro, Pwani, Iringa, Mbeya, Ruvuma , Kilimanjaro, Tanga na Singida.
MWANANCHI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha kwa muda uandikishaji wa wapigakura katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani hadi hapo itakapotangazwa.
Uandikishaji huo unaofanywa kwa teknolojia inayochukua alama na taswira za mpigakura ‘Biometric Voters Registration’ (BVR)) ulipangwa kuanza Julai 4 hadi 16 kwa Dar es Salaam na Juni 25 kwa Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba alisema jana kuwa kazi hiyo imeahirishwa kutokana na kuchelewa kwa vifaa vinavyotumika kuandikisha wapigakura.
Alisema vifaa vilivyokuwa vinakusudiwa kutumika Dar es Salaam bado
vinatumiwa katika mikoa ambayo wananchi wamejitokeza kwa wingi
kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.
“Mwitikio umekuwa mkubwa ndiyo
maana tumeamua kusogeza mbele tarehe ili wamalizie huku tukiendelea
kusubiri vifaa. Tunataka vikija tuishambulie Dar es Salaam kwa kipindi
kifupi,” Mallaba.
Mallaba alisema tarehe ya kuanza tena kwa kazi hiyo kwa mikoa ya Dar
es Salaam na Pwani itatangazwa na NEC baada ya kupata vifaa kutoka mikoa
itakayokuwa imekamilisha uandikishaji.
“Ninaomba wananchi wafahamu
kuwa mwezi uliokuwa umepangwa na NEC kukamilisha zoezi hilo utabaki kuwa
Julai. Tarehe tu ndiyo itabadilika,” alisema na
kusisitiza kuwa wanataka uandikishwaji kwa jiji hilo uwe wa kipekee
ukiwa na vifaa vya kutosha kutokana na idadi kubwa ya watu. Aliwataka
wananchi wote wa mikoa hiyo miwili kuwa watulivu wakati huu.
Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika alisema NEC imedhihirisha hoja aliyowahi kuitoa bungeni kwamba Bunge liahirishwe ili wajadili suala hilo kwa dharura.
“Kuna udhaifu mkubwa kwa upande
wa NEC na Serikali kuhusu BVR… hata baada ya madai kwamba umerekebishwa
lakini ukweli ni kwamba hali ni tete hata katika maeneo mengine ambayo
uandikishaji unaendelea,” Mnyika.
Alieleza kuwa Dar es Salaam ndiyo itakayoamua mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kutoka na idadi kubwa ya wapigakura.
Alidai kwamba kubadilishwa huko kwa ratiba kutatoa mwanya kwa CCM ambayo ilishasema kupitia kwa Nape Nnauye kuwa inajiandaa kufunga goli la mkono kufanya hujuma.
MWANANCHI
Mahakama ya Mkazi Kisutu jana ilishindwa kutoa hukumu ya kesi ya wizi
wa milioni 207 kutoka kwenye akaunti ya madeni ya nje EPA kutokana na
mshtakiwa wa tatu kulazwa katika hospitali ya Muhimbili, kitengo cha
wagonjwa wa akili.
Hukumu ya kesi hiyo inayowakabiliwa makada watatu wa CCM, Rajabu Maranda na wenzake wanne, sasa itasomwa kesho kutokana na kulazwa kwa mtuhumiwa huyo, Iman Mwakosya ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha madeni ya nje cha benki kuu ya Tanzania.
Wengine kwenye jopo hilo ni Ignas Kitusi na Eva Nkya.
Mahakama itaandika barua kwa hospitali ya Muhimbili kabla ya Julai
Mosi kwa ajili ya kupata taarifa kama mshtakiwa huyo anaweza kuelewa
mwenendo wa kesi ili waweze kusoma hukumu.
NIPASHE
Magonjwa yasiyoambukiza yakiwamo ya kisukari, moyo na saratani,
yanazidi kuongezeka kwa kasi na kuendelea kuwa chanzo kikuu cha vifo
duniani kote.
Aidha, inakadiriwa kuwa kisukari pekee kimeathiri maisha ya watu
takribani milioni 371 duniani kote huku asilimia 80 ya idadi hiyo
ikiishi katika nchi zenye uchumi wa kati na maskini.
Nchini Tanzania, takribani watu tisa kati 100 wana ugonjwa wa
kisukari na kwamba mtu mzima mmoja kati ya watatu, ana tatizo la
shinikizo la juu la damu.
Kaimu Mkurugenzi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Hauson Rweumbiza, alisema wakati wa semina ya siku moja iliyowashirikisha waandishi wa habari wa kutoka vyombo mbalimbali.
Lengo la semina hiyo lilikuwa ni kuzungumzia magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.
Alisema gharama ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza
duniani kote ni mabilioni ya dola na hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa
rasilimali finyu zilizopo.
“Kwa mwaka 2010, Shirika la
Afya Duniani lilikadiria kuwa jumla ya gharama zinazohusiana na kisukari
zilifikia Dola bilioni 378 duniani kote na kiasi hicho cha fedha
kinaweza kufikia Dola bilioni 490 ifikapo mwaka 2030,” alisema.
Naye Mratibu kutoka Taasisi ya Kisukari hapa nchini,
John Gadina,
alisema utafiti uliofanyika mwaka 2012, ulionyesha kuwa asilimia tisa
ya Watanzania waligundulika kuwa na kisukari huku Wilaya ya Temeke
ikiongoza.
Alisema ugonjwa huo umewakumba vijana na watu wenye umri mkubwa na
kwamba serikali mpaka sasa imefikia kutoa huduma hiyo kwa asilimia 75
ambapo kila palipo na hospitali panakuwa na kitengo cha kutoa huduma za
ugonjwa huo.
Alisema sababu ya Wilaya ya Temeke kuwa na wagonjwa wengi imetokana
na ulaji kwa wingi wa vyakula vya nazi, chapati, wali pasipo kufanya
mazoezi.
JAMBOLEO
Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya
kijamii, kuwa kuanzia kesho na keshokutwa kutakuwa na uhaba wa mafuta
kwenye vituo vya kuuza mafuta.
Kauli hiyo ya kukanusha imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Charles Mwijage wakatia kijibu swali lililoulizwa na
Job Ndugai jana Bungeni, Dodoma.
Ndugai alimtaka Waziri kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa ambazo
zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kaunzia kesho kutakua na
tatizo la upatikanaji wa mafuta na kusababisha shughuli nyingi kusimama.
Mwijage alisema taarifa ambazo wanazo kama Wizara ni kuwa hifadhi ya
mafuta ipo ya kutosha na kuwa uhaba wa mafuta hauwezi kutokea kwa kuwa
wana uhakika kuwa mafuta yapo ya kutosha.
Alisema hata yeye ameonakwenye mitandao ya kijamii na sasa wanafuatilia ili kujuab chanzo cha taarifa hizo ni nini.
lisema iwapo kuna msambazaji au mfanyabiashara atajaribu kufanya
hivyo kanuni kanuni na sheria zilizopo zitatumika kuhakikisha wahusika
wanawajibishwa.
HABARILEO
Walimu wawili wapya wa Shule ya Msingi
Sang’ang’a kata ya Pemba tarafa ya Inchugu wilayani Tarime, mkoani Mara
wanashikiliwa nchini Kenya kwa kosa la kuingia nchini humo bila kuwa na
kibali.
Walimu hao wawili ambao ni Ahedius Orio kutoka mkoa wa Kilimanjaro na mwenzake Elias Nandi kutoka Lindi wanashikiliwa na polisi nchini Kenya walipokwenda nchini humo kwa matembezi.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Sweetbard Njewike
alithibitisha kukamatwa kwa walimu hao wawili wapya wa shule ya msingi
Sang’ang’a iliyopo umbali wa kilometa moja kutoka mpakani mwa Tanzania
na Kenya.
Kamanda huyo alisema walimu hao katika
kipindi hiki cha likizo, mwishoni mwa wiki waliamua kwenda kutembelea
kijiji jirani cha Nyametaburo Kipimo ambacho kiko upande wa Kenya.
Alisema wakati wakiwa kijijini hapo
walikutwa na Polisi wa nchi hiyo na kuwapeleka, kituo cha Polisi na
Uhamiaji cha Isebania kuwahoji ambapo ilidaiwa waliingia nchini humo
bila ya kufuata taratibu za kuwa na vibali vya kuingia nchini humo.
“Tumewasiliana
na wenzetu wa nchini Kenya ambapo wamedai kuwapeleka mahakamani kujibu
shitaka la kuingia nchini humo bila vibali na wanatakiwa ndugu zao ama
marafiki wakawadhamini huku juhudi za kuwasaidia walimu hao zinafanyika
ili waweze kuachiliwa,” Njewike.
Awali habari zilizotangazwa na vyombo
vya habari vya Kenya, ikiwemo televisheni na redio za Citizen
zilitangaza kuwa walimu hao walidaiwa kuwakusanya na kuwashawishi vijana
wakiwemo kutoka Tanzania na Wakenya kujiunga na vikundi vya kigaidi vya
al Shabaab.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog