Mauaji yazua mjadala wa ubaguzi US
Matumizi ya neno ''uhalifu wa chuki'' ili kuelezea mauaji ya watu tisa katika
kanisa moja la watu weusi mjini Carolina Kusini nchini Marekani umezua
mjadala kuhusu ni nini haswa kinachosababisha mtu kutekeleza ugaidi.
Watu
wengi wameonyesha hasira zao kuhusu afisa mkuu wa polisi mjini
Charleston alivyoelezea kisa hicho wakati wa mkutano na vyombo vya
habari.Mshukiwa Dylan Roof , mwenye umri wa miaka 21 ameshtumiwa kwa kuingia ndani ya kanisa saa tatu za usiku siku ya jumatano na kuwapiga risasi waumini waliokuwa katika maombi.
Kanisa la Kiafrika la kimethodisti lina historia ndefu kama eneo la vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na ni muhimu katika historia ya Wamarekani weusi.
Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment