Siku 1 jela kwa kukojoa hadharani India
Watu 109 wamehukumiwa kifungo cha siku moja jela kwa kukojoa hadharani huko India.
Polisi waliwakamata takriban watu 109 kwa kukojoa katika vituo vya usafiri wa umma na reli.Wale wote waliokamatwa wanatuhumiwa kwa kupatikana na hatia ya kukojoa nje ama ndani ya vituo vya reli mjini Agra Kaskazini mwa India .
Waliokamatwa watahukumiwa kifungo cha saa 24 ama walipe faini ya kati ya dola mbili na kumi au vyote.
Mkuu wa polisi katika eneo hilo GRP, Gopeshnath Khanna aliyeongoza operesheni hiyo anasema kuwa itaendelea hadi wahindi wanaolaumiwa kwa kuharibu mazingira kwa kutema mate ukutani baada ya kutafuna thambuu na tumbako iliyowekwa rangina kukojoa katika maeneo ya umma watakapo badili tabia zao.
Aidha wasafiri wa reli wanasemekana kupigwa na harafu mbaya ya mkojo pindi wanapoingia ndani ya vituo hivyo.
Takwimu za afya nchini humo zinaonesha kuwa takriban watu milioni mia sita 600m ama nusu ya raia wa India hawana vyoo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment