Kiongozi wa ujasusi wa Rwanda, Luten Jeneral Karenzi Karake ameachiliwa kwa dhamana.
na kutakiwa kufika kwenye kituo cha polisi kila siku alikamatwa siku ya Jumamosi katika
uwanja wa ndege wa Heathrow Jumamosi iliyopita chini ya kibali cha ulaya. ametakiwa na Madrid
kuhusiana na vifo vya wafanyikazi wahispania waliokuwa wakihudumia
mashirika ya misaada na mauji ya kimbari nchini Rwanda.
. Jenerali Karenzi Karake,
mwenye umri wa miaka 54 ni mtu wa kwanza wa ngazi ya juu kutoka kwa
orodha ya watu 40 walio na wadhfa mkubwa katika jeshi la RPF orodha
iliyotolewa na jaji mmoja wa Uhispania akitaka wakamatwe. Wanakabiliwa na mashtaka ya
madai ya kuhusika katika vitendo vinavotajwa kuwa uhalifu wa kivita
uliofanyika dhidi ya Wahutu mnamo mwaka 1990 huko Kazkazini mwa Rwanda.
Miongoni
mwa wanaodaiwa kufariki kutokana na matukio hayo ni raia watatu wa
Uhispania waliokuwa wakifanya kazi ya kutoa misaada ya kibinadamu katika
eneo hilo la kazkazini mwa Rwanda. Jaji Muhispania Fernando Merelles ndiye aliyetoa warranti hizo na kutaka wakamatwe,agizo alilolitoa tangu February 2008 . Serikali ya Rwanda imeghadhabishwa na waranti hizo ikisema hazina msingi wowote.
Rwanda
imekuwa ikishtumu hatua hiyo ya jaji Merelles na kusema ni kutumiwa
vibaya na mahasimu wa Serikali wenye misimamo mikali na kwamba
Jaji huyo hajachukua hatua zipasavyo kupata mashahidi kutoka Rwanda au hata kufanya kazi pamoja na mahakama za Rwanda.
Kwa habari, amatukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment