Baada ya Mbrazil Firmino, Liverpool sasa inajipanga kumchukua huyu mwingine !!
Liverpool walituma ofa ya Paundi Milioni 12.5 kwa ajili ya Clyne, na baada ya Southampton kuikubali sasa hivi kilichobakia ni suala la vipimo vya afya ili mchezaji huyo ajiunge na Kikosi hicho.
Clyne ambaye yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Southampton kwa sasa yupo mapumzikoni na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka 5 ikiwa atafuzu vipimo vya afya.
Kama usajili ukikamilika mchezaji huyu atakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool katika dirisha hili la usajili, ambapo ataungana na Firmino aliyetua Anfield kwa ada ya Paundi Milioni 29… Wachezaji wengine waliosajiliwa ni James Milner, Adam Bogdan na Joe Gomez.
Kwa habari, amtukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment