Hadi kufikia September 2013 hizi ni hoteli 10 zinazotajwa kuwa na muonekano usio wa kawaida
1- Grand Lisboa Hoteli
Grand
Lisboa Hoteli hii ni hoteli ambayo ipo Macau China, jengo lake lina
urefu wa mita 258, upekee wa jengo hili limejengwa katika muundo wa ua
ambalo kwa juu linachanua.
3- Ryugyong Hoteli
Ryugyong
Hoteli ipo Korea Kaskazini ni jengo lenye muundo wa Pyramid lakini sifa
yake nyingine ni kuwa limejengwa kwa muda mrefu toka mwaka 1987 ndio
lilianza kujengwa ila hadi September 2013 bado ilikuwa inaripotiwa kuwa
linaendelea kujengwa.
5- Inntel Hoteli
Inntel
Hoteli iliyopo Uholanzi hii imejengwa kwa muundo wa nyumba za asili ya
kidachi yaani kijumba kimoja kimejengwa juu ya kingine.
Aviator Hoteli ipo Uingereza imeingia katika hii list kwa kuwa wameitaja kuwa na muonekano wa ndege.
Burj
al Arab hii ipo Dubai mtu wangu imejengwa kwa muundo wa lile pazia
ambalo linatumika kuongozea ngalawa ambazo zilitumiwa na waarabu kuja
Afrika.
Taj Lake Palace Hoteli ipo India mtu wangu upekee wake ni kuwa muonekano wake ni kama inaelea kati kati ya ziwa.
10- Hotel Marqués de Riscal
Hotel
Marqués de Riscal mjengo wa hoteli hii ya Hispania, muonekano wake ni
ngumu kulinganisha na kitu ila umepambwa kwa rangi flani hivi za
kinywaji cha wine.
No comments:
Post a Comment