Arsenal walala 2-1 mbele ya Everto
Arsenal wamepoteza nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya Everton kutoka nyuma na kuondoka na ushindi wa 2-1.
Washika
bunduki hao walishinda michezo mitatu mfululizo walianza vyema katika
mchezo dhidi ya Everton baada ya Alexis Sanchez kupiga safi mkwaju wa
adhabu nje kidogo ya eneo la hatari uliombabatiza mlinzi Ashley Williams
na kuingia wavuni.Kipindi cha pili kila timu ilirejea kwa lengo la kuchukua alama tatu lakini ni Everton ndio waliofanikiwa baada ya Williams kufuta makosa yake kwa kuifungia Everton goli la pili na la ushindi.
Nahodha wa timu ya Everton Phil Jagielka alitolewa kwa kadi nyekundu dakika chache tu kabla ya kumalizika kwa mchezo huo baada kupata kadi ya pili ya njano.
Everton wanabakia nafasi ya saba wakiwa na alama 23.
No comments:
Post a Comment