Mashua s
iliyotengenezwa katika mji mkuu wa Belfast huko Ireland ya Titanic
itawekwa katika eneo la kumbukumbu la theme park nchini India.
Ujenzi
huo wa mashua hiyo yenye urefu wa kina cha mita 269, itawekwa katika
hifadhi iliyoko mashambani , katika mkoa wa Sichuan, .
Ujenzi huo uliaza siku ya Alhamisi.
Mashua
ya Titanic iliyojengwa na Harland na Wolff huko Belfast , iligonga
mwamba wa barafu na kuzama Kaskazini mwa Atlantic mwaka 1912 hatua
iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,500.
Mashua hiyo ilikuwa katika safari yake kutoka Southampton ikielekea New York.
Habari kuhusu meli hiyo ni swala ambalo liliwashangaza raia wengi kutoka China. Muelekezi wa filamu, James Cameron, kutoka Canada,
alikuwa na mashua kama hiyo iliotengezwa kwa maswala ya uigizaji pekee ,
lakini hakuna mashua sawia na hiyo iliowahi kutengenezwa.
Bilionea
mmoja kutoka Australia, Clive Palmer, alitangaza mipango yake ya
kutengeneza mashua kama ya Titanic mwaka 2012, lakini mradi huo bado
haujakamilika. Meli hiyo ya China, itakuwa yenye umbo sawa na ile
ya Titanic , itakuwa na sehemu ya michezo, maonyesho, kuogelea na
sehemu maalum ya watu maalum ambayo itakuwa na mtandao wa Wifi na
inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika eneo hilo la theme park lililoko
kilomita kadhaa kutoka pwani ya China.
No comments:
Post a Comment