Barua ya Mohammad Ali kwa Mandela yauzwa paund 7,200


Barua iliyowekwa
sahihi na mwanamasumbwi Mohammad Ali na kuandikiwa rais wa zamani wa
Afrika Kusini Nelson Mandela, akitoa rambu ramba zake kufuatia kuawa
kwa mtu aliyekuwa akipinga ubaguizi wa rangi imeuzwa kwa pauni 7,200.
Muuzaji
wa barua hiyo Andrew Aldridge alisema, "ni vyema kuwa Mohammad Ali
alikuwa mwanamichezo bora zaidi hukui naye Nelson Mandela akiwa mtu
mashuhuri zaidi katika karne iliyopita.
Barua hiyo ilipiwa chapa cha msaidizi wa meneja wa hoteli ya Elangeni iliyo mjini Durban ambapo Ali alikuwa akiishi wakati huo.
Barua hiyo iliyouzwa kwa mnunuzi kutoka nchini Marekania ilitarajiwa kuuzwa kwa kati ya dola 6,000 na 8,000.
BBC
No comments:
Post a Comment