Je Di Maria anaondoka Man Utd, kituo cha TV cha mmiliki wa PSG kina majibu haya.
Tetesi za usajili wa kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Angel Di Maria kuondoka Old Trafford na kujiunga na Paris Saint Germain leo zimechukua sura mpya.Akiwa na miaka 27, Manchester United walivunja rekodi ya usajili ya Uingereza kwa kulipa kiasi cha £59.7m kumsajili Angel Di Maria lakini muargentina huyo ameshindwa kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu ya EPL na inaaminika anavutiwa na wazo la kwenda PSG.
Hata hivyo, inaonekana vilabu hivyo vimeshindwa kuafikiana juu, huku CEO wa United akiripotiwa kutaka kurudisha fedha zote walizotumia kumpata winga huyo.
No comments:
Post a Comment