Ziara ya Obama:Anga ya Kenya kufungwa
Shirika
linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga
ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii
ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja
wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.
Kwa mujibu
wa shirika hilo, agizo hilo litatekelezwa katika viwanja vyote vya ndege
nchini Kenya na kuwa anga hiyo itafunguliwa muda tu pale ndege hiyo ya
rais Obama itakapokuwa imetua.Shirika hilo limesema kuwa limeyaandikia mashirika yote ya ndege na pia kampuni zote za usafiri kuhusiana na agizo hilo na kuwa safari za ndege kadhaa zitacheleweshwa siku hiyo na pia siku ya jumapili wakati rais Obama atakapokuwa akiondoka nchini Kenya kuelekea Ethiopia kwa muda wa dakika arubaini.
Agizo hilo sasa linamaanisha ndege zote ndogo ndogo ambazo uhudumu kati ya Nairobi na Somalia na viwanja vingine vidogo vidogo katika kanda ya Afrika Mashariki, havitaruhusiwa kutua Nairobi hadi mkutano huo utakapomalizika.
Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa mjini Nairobi siku ya Ijumaa usiku ambapo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano hilo la kibiashara kwa pamoja na mwenyeji wake rais uhuru Kenyatta.
Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment