Club ya Simba SC kwenye headlines moja na Real Madrid, Barca na Manchester United.

Kila mwaka klabu ya
Simba
huwa na utamaduni wa kufanya tamasha la kutambulisha jezi, wachezaji na
mipango mingine ya klabu hiyo.Tamasha hilo linalojulikana kama
Simba Day kwa mwaka huu haitakuwa
Simba Day bali ni wiki ya
Simba. Mabadiliko hayo yametokana na maboresho kadhaa ambayo yamefanywa na uongozi.

Uzinduzi huo utafanyika siku ya Jumamosi August 1 katikati ya jiji la
Dar Es Salaam saa 4:30, kwa mujibu wa mkuu wa idara ya habari ya
Simba, Haji Manara amethibitisha kufanyika kwa mambo mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa maduka yatakayouza jezi za
Simba,
mabegi, kalamu, kofia na vitu vingine mbalimbali vyenye logo ya Simba
ikiwa ni sehemu nyingine ya kuuongeza uchumi wa club.
Manara amethibitisha kuwepo kwa maduka ya bidhaa za klabu sehemu mbalimbali ikiwemo
Mlimani City, huku kilele cha Wiki ya
Simba itakuwa August 8 Uwanja wa Taifa
Dar Es Salaam kwa
Simba kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya
FC Leopard ya
Kenya. Hata hivyo
Manara amekanusha madai yanayosambaa kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa
Burundi Laudit Mavugo hatokuja
Simba.
“Mavugo nimeona kwenye gazeti nimesikitishwa sana, wiki iliyokwisha gazeti hilohilo liliandika Okwi
anarejea Msimbazi hata chezea tena klabu yake ya Denmark wakaandika
bila kuweka source bila kubalance story nawahakikishia Mavugo siku ya
tarehe 8 August atacheza mechi ya Simba day “>>> Haji Manara
Ungana nami kwa habari motomoto za papo kwa papo , ni ha hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment