Manchester United ilivyoiadhibu FC Barcelona July 25

Usiku wa Leo wa kuamkia July 26 vilabu viwili vikubwa barani
Ulaya vilikutana kucheza mchezo wa
International Champions Cup,
michuano ambayo bado inaendelea katika nchi mbalimbali na sehemu
zingine kumalizika…Michuano hii ambayo klabu nyingi hutumia kama sehemu
ya maandalizi ya msimu mpya ya Ligi Kuu katika nchi zao, usiku wa July
25 kuamkia July 26 umezikutanisha timu za
FC Barcelona ya
Hispania dhidi ya
Manchester United ya
Uingereza.
Mchezo huo umepigwa katika Uwanja wa Levi’s Stadium California Marekani hadi dakika 90 zinamalizika Manchester United imeibuka na ushindi wa goli 3-1 magoli yakifungwa na Wayne Rooney dakika ya 8, Jesse Lingard dakika ya 65 na Adnan Januzaj dakika ya 91 huku goli pekee la kufutia machozi kwa FC Barcelona likifungwa na Rafael Rafinha dakika ya 90.

Hii sio mara ya kwanza kwa klabu za
FC Barcelona na
Manchester United kucheza mechi ya kirafiki kama hiyo ya
International Champions Cup 2015, kwani iliwahi kukutana mwaka 2011 na
Man United kuibuka mshindi kwa goli 2-1 kabla ya mwaka 2012 kukutana tena na
FC Barcelona kushinda kwa mikwaju ya penati.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment