Hakuna anayeogopa mafuriko au? Watu na maisha yao, nyumba zinaelea juujuu ya maji… (Pichaz)
Karibu mtu wa nguvu ambaye unavutiwa na
pichaz za mijengo mikali kabisa… unajua ni kitu kinachovutia pia wakati
mwingine kuona watu wakiwa na mijengo yao ambayo iko tofauti kabisa na
aina ya nyumba tulizozoea, pata picha inavyokuwa noma ikitokea ishu kama
mafuriko alafu hapohapo unaambiwa kuna watu wamejenga juu ya maji na
wanaishi kwa amani kabisa !!
Usishtuke
kuona inaelea mtu wangu, huu ndio muundo ambao wataalam wanasema kama
unataka nyumba yako iwe inaelea itabidi ijengwe hivyo… chini yake
kunakuwa na kitu kama boya lililojaa hewa, ndio kinachofanya na nyumba
ielee juujuu.
Nimezipata picha nyingi kabisa mtu
wangu, unaambiwa kwa Marekani kwenye Miji kama ya Seattle na Portland
hii ni kawaida kabisa kukutana nayo…. cheki watu na maisha yao mengine
kabisa na nyumba zao juu ya maji bila hofu !!
Unayashangaa ya nyumba kuelea? hapa ni mtaa mzima uko juujuu !!
Umewahi kushuhudia mafuriko? Vipi ikitokea unapewa moja ya hizi nyumba uishi utakubali??
Nitakutumia stori zote zinazonifikia hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment