TANGA KUMEKUCHA

Wednesday, July 22, 2015

HADITHI SEHEMU YA (8)


hadithi



 
NILIJUA NIMEUA 8
 
ILIPOISHIA
 
“Nzuri Zacharia. Kumbe unaishi Zanzibar?”
 
“Nilienda kwa muda, niko Dar”
 
“Kikazi uko wapi?”
 
“Baada ya kuchukua shahada yangu ya sheria niliajiriwa na Wizara ya mambo ya nje”
 
“Nimefurahi kukuona, karibu tena Tanga”
 
“Asante. Nahitaji teksi ya kunipeleka mjini”
 
“Mimi pia ni dereva wa teksi. Hapa nimefuata abiria”
 
“Kumbe unaendesha teksi! Vizuri sana. Basi twenzetu”
 
Nikatoka naye. Mara tu baada ya kujipakia kwenye teksi mazungumzo yakaanza.
 
“Ajira zimekuwa ngumu sana. Nimeangukia kwenye udereva” nilimwambia Zacharia wakati nikiiwasha teksi.
 
SASA ENDELEA
 
“Kwa sasa hivi sekta binafsi ndio kimbilio la watu wengi. Hata mimi kuna uwezekano mkubwa nikaacha kazi na kujiajiri mwenyewe”
 
“Wewe mwenzetu una shahada yako ya sheria, unaweza kujiajiri mwenyewe. Taabu ni kwetu sisi tulioishia sekondari”
 
“Hapana. Ajira ni ajira tu. Hata kuendesha teksi ni ajira, ilimradi tu unapata riziki yako na maisha yanakwenda. Kwani teksi ni ya kwako mwenyewe?”
 
“Hapana si yangu”
 
“Lakini masilahi yapo”
 
“Nashukuru, si sawa na kukosa kabisa”
 
“Mimi nataka kuwa wakili wa kujitegemea. Nitakuja kufanya kazi zangu hapa Tanga”
 
“Itakuwa vizuri sana. Huduma ya uwakili inahitajika sana na katika mkoa wetu  tuna mawakili wachache sana”
 
“Pengine mwakani nitakuwa nimeshapata leseni”
 
“Nakuombea mafanikio. Unakwenda wapi?”
 
“Mtendele Hotel”
 
“Pale Chuda?”
 
“Ndiyo Chuda. Nitakuwa pale kwa wiki moja hivi”
 
“Zanzibar ulifuata nini?”
 
“Nilienda kikazi”
 
‘Tulifika Mtendele Hotel. Wakati anashuka alinikaribisha. Na mimi nikashuka na kumfuata.
 
“Hatuwezi kuachana haraka. Hatujakutana miaka mingi” aliniambia wakati tunapenya katika lango la hoteli hiyo mpya.
 
Wakati anaandikisha chumba aliniambia nikae kwenye kiti, akaniagizia bia.
 
Alipopatiwa chumba alirudi tukaakaa sote. Na yeye akaagiza bia. Tulikunywa huku tunazungumza hadi nikakata chupa nne. Baada ya kulipia bia tulizokunywa alinipa shilingi laki mbili.
 
“Chukua hizo rafiki yangu” akaniambia. Nikamshukuru sana.
 
“Nipatie namba yako ya simu ili kama nitahitaji teksi nikuite” akaniambia.
 
“Sawa”
 
Nikampa namba yangu na yeye akanipa yake. Tukaagana na nikamuacha hapo hoteli.
 
Nilirudi nyumbani kwangu kwenye saa mbili usiku. Kwa vile nilipewa laki mbili na Zacharia, sikutaka kuendelea na kazi usiku. Niliona nirudi nyumbani nilale.
 
Lakini nilipofika nyumbani mke wangu aligundua kuwa nilikuwa nimelewa.
 
“Unatoka wapi?” akaniuliza.
 
Nikamueleza kuwa ukweli.
 
“Na mimi nataka. Nenda kanunue zingine tuje tunywe” akaniambia.
 
Sikubishana naye. Nikatoka na kujipakia kwenye teksi yangu. Dakika chache tu baadaye nikarudi nikiwa na makopo sita ya bia.
 
Kwanza tulikula chakula cha jioni. Baada ya kula tukaanza kunywa. Tuliendelea kunywa hadi saa sita usiku.
 
Kabla hatujamaliza bia zetu tulisikia kishindo kilichotokeaa uani. Baadaye tulisikia kama kulikuwa na mtu anatembea.
 
“Hebu nenda uko uani, isijekuwa mwizi ameingia” Halima akaniambia.
 
Nikanyanyuka. Nilikuwa nimelewa sana kwa vile sikuwa na uzoevu wa kunywa bia mara kwa mara.
 
“Chukua panga usiende mikono mitupu”
 
“Panga liko wapi?”
 
Halima akanipatia panga hilo. Nikalishika na kutoka nalo uani. Kwa vile taa ilikuwa inawaka nliweza kuona bila matatizo. Kwanza sikuona kitu. Nikawa natafuta tafuta kwenye vipembe.
 
Ghafla taa ya uani ikazimika. Nikashituka na kujiuliza nani amezima taa? Ikabidi nirudi ndani haraka kwani kama kulikuwa na mtu mbaya amejificha sehemu angeweza kunishambulia.
 
Kwa vile kulikuwa na giza sikuweza kuona mbele, nikajigonga na pipa la maji lililokuwa mbele yangu. Kwa vile nilikuwa nimelewa ilibaki kidogo tu nianguke chini. Wakati nasepetuka nikahisi kitu kikinivamia nyuma yangu. Nikashituka na kudhani ni mwizi alikuwa anataka kunishambulia.
 
ITAENDELEA KESHO na usikose nini kitajiri katika sehemu ya 9 ya hadithi hii hapa hapa tangakumekuchabliog
Imechapishwa na Unknown kwa 3:28 AM
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Time

 Time in Tanga

Total Pageviews

619,652

My Blog List

Blog Archive

  • ►  2014 (563)
    • ►  November (97)
    • ►  December (466)
  • ▼  2015 (3131)
    • ►  January (417)
    • ►  February (332)
    • ►  March (351)
    • ►  April (308)
    • ►  May (263)
    • ►  June (255)
    • ▼  July (260)
      • BAYERN MUNICH WAANZA NA KICHWA HIKI
      • VA GAAL AONYESHA MAKEKE
      • WATU 27 WAUWAWA KWA BOMU UTURUKI
      • REAL MADRID YAKWAA KISIKI KWA GEA
      • SEPP BLATTER AFANYIWA DHIHAKA MBLE YA USO WA DUNIA
      • MWENGINE AJITOKEZA KUMPOSA MALIA OBAMA
      • BIASHARA VINYAGO, TANGA
      • SANGOMA ALINENA , YALITIMIA
      • SOMA HABARI KUBZWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LE...
      • MOURINHO AMUONEA GERE CASILLAS
      • MPINZANI WA MANNYWEATHER AMETAMBULIKA, HUYUO HAPA
      • FURAHA YA IDD EL FITRI TANGA
      • VAN GAAL NA MIPANGO YA KUMYAKUA MWANANDINGA HUYU
      • RAHEEM STERLING AANZA KWA KUIFUNGIA TIMU YAKE MPYA
      • VIWANJA 10 VILIVYOJENGWA KWA GHARAMA KUBWA ZAIDI D...
      • UJIO WA OBAMA KENYA SIO MCHEZO, CHEKI MADEGE YA AJ...
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • AZAM YASAJILI WENGINE WA KIGENI
      • MASTAA 10 ZA PESA ZAO
      • HADITHI SEHEMU YA (8)
      • NAIROBI KUMEKUCHA, HAKUNA KULALA
      • KUSIKIA OBAMA HATOPITIA CHUONI KWAO, UAMUZI WALIOU...
      • YASIKUPITE MAGAZETI YA LEO, JULY 22 TZ
      • MTAA WAFANYWA DAMPO LA TAKATAKA, TANGA
      • 50 CENT KWELI NI FUKARA?
      • WASHABIKI WA CHALSEA WALIOMYANYIA UBAGUZI KIJANA M...
      • MWANAFUNZI APOTEZA MAISHA AKIFANYA MCHEZO NDANI YA...
      • CCM VITI MAALUMU UDIWANI TANGA KUMEKUCHA
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • TEMBEA UONE USINGOJE KUHADITHIWA
      • CHALSEA YAANZA MICHUANO YA CAPITAL ONE VIBAYA
      • ZLATAN IBRAHIMOVIC AHUSISHWA KUREJEA AC MILAN
      • ANGA YA KENYA KUFUNGWA KWA DAKIKA 50 KUPISHA NDEGE...
      • MAMBO YAZIDI KUNOGA NAIROBI UJIO WA OBAMA
      • DI MARIA HUYOOOOO PSG
      • MASUPA STAA KUTOKA UTOTONI HADI UKUBWANI
      • ARSENAL WENGER KIGUGUMIZI
      • MAAJABU NA KWELI
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • AUWA WAWLI NA YEYE KUJIMALIZA
      • SPAIN YAONGEZA MIAKA UMRI WA KUOANA
      • SZEKO KUTIMKA MAN CITY
      • WACHEZAJI FC BARCELONA WAVINJARI NA WACHEZAJI WA N...
      • AMINI USIAMINI BEACH NDANI YA NYUMBA
      • SUNDAY OLISE AMUITA MIKEL OBI WA CHALSEA KUMENYANA...
      • VIBOPA WA ARSENAL WAMTAKA WENGER KUVUNJA SANDUKU L...
      • KOREA KILA MFANYAKAZI ATAKIWA KUFIKA SAA 11 ALFAJIRI
      • KILICHOWAKUTA MAN CITY MBELE YA REAL MADRID
      • NAIROBI, NI OBAMA TU
      • NKURUNZINZA AIBUKA MSHINDI, ARUDI IKULU
      • OBAMA KUZUNGUMZA NA WAJASIRIAMALI LEO
      • WAMASAI KUNOGESHA ZIARA YA OBAMA KENYA
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • OBAMA FURAHA TUPU MARA BAADA YA KUONA NA DADA ZAKE
      • JE, UNAJUA ARSENAL ILIWAHI KUZAWADIWA KOMBE LA DHA...
      • KONA ZOTE NI RONALDO NA MTOTO WAKE TU
      • AZAM YATINGA ROBO FAINAL
      • OBAMA AKUTANA NA RUTO ANADAIWA KUWA NA KESI ICC
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • MAN UNITED YAITANDIKA BARCELONA , MICHUANO YA INTE...
      • OBAMA HATAZURU KABURI LA BABA YAKE
      • GULIO LA TANGAMANO, TANGA
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • SNOOP DOG ABAMBWA NA UNGA SWEDEN
      • MANCHESTER UNITED YAZIDI KUKIMARISHA KIKOSI CHAKE
      • CANDLE EDUCATION CENTRE TANGA HAIJAKUKOSESHA MAGA...
      • OBAMA AIONYA ETHOPIA , HAKI ZA BINADAMU
      • SIMANZI
      • MTOTO ANYWESHWA MAZIWA YALIYOCHANGANYWA NA POMBE
      • DROBA AIBUKIA MAREKANI
      • RONALDO NA MESSI
      • PANGANI WALIA NA UKUTA MTO PANGANI
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • MORINHO NA KAULI ZAKE, LEO KATIKA HEAD LENE NYENGINE
      • MTOTO WA RAIS WA ZAMANI WA LIBYA AHUKUMIWA KUNYONGWA
      • UCHAGUZI WA FIFA MWAKANI
      • LOWASSA AIBUKUA UKAWA
      • VIDAL AIBUKIA BARYEN MUNICH
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • AIRTEL YABORESHA HUDUMA ZAKE TANGA (YAZINDUA KITUO...
      • NCHI ZINAZONGOZA KWA UBAKAJI DUNIANI
      • AZAM YAITANDIKA YANGA MIKWAJU YA PENALTI
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • KAMA HUJAKUTANA NA AJALI KAMA HIZI, UZIOMBE YAKAKU...
      • DI MARIA KIZUNGUZUNGU
      • SOMA KURASA MWANZO MWISHO YA MAGAZETI YA LEO, JULY...
      • MARADONA VITUKO HADI MITAANI
      • CHEMCHEM ILIYOSAHAULIKA KIJIJI CHA MAJIMOTO AMBONI...
      • FACE BOOK KIDEDEA
      • VIMBWANGA VYA WALIMWENGU
      • WANAOFANYA MGOMO WA KULA GEREANI ISRAEL , KUKIONA
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • UZI WA STAND UNITED HUU HAPA
      • OBAMA ZAWADI ZA KENYA HAKIONDOKA NAZO
      • WAKALI KUPEPETANA WEMBLEY
      • MASTAA WA LIVERPOOL WAKIJINOA
      • AZAM YATINGA NUSU FAINAL
      • MABILIONE 5 LIGI KUU UINGEREZA
      • KIPENGA FOMU ZA URAIS CHAPULIZWA
      • UZINDUZI JEZI MPYA YA SIMBA NA MADUKA YAKE LEO
    • ►  August (246)
    • ►  September (237)
    • ►  October (210)
    • ►  November (142)
    • ►  December (110)
  • ►  2016 (1913)
    • ►  January (121)
    • ►  February (102)
    • ►  March (131)
    • ►  April (198)
    • ►  May (196)
    • ►  June (197)
    • ►  July (197)
    • ►  August (186)
    • ►  September (159)
    • ►  October (160)
    • ►  November (138)
    • ►  December (128)
  • ►  2017 (562)
    • ►  January (134)
    • ►  February (106)
    • ►  March (113)
    • ►  April (77)
    • ►  May (72)
    • ►  June (11)
    • ►  September (1)
    • ►  October (36)
    • ►  November (10)
    • ►  December (2)
  • ►  2018 (1)
    • ►  February (1)
Picture Window theme. Powered by Blogger.