Utatamani kuyaona mazuri ya Nigeria 2016? Na huu mjengo kama wa Marekani utakuwepo !!
Kwenye list ya nchi ambazo zina uchumi
mzuri zaidi Africa, Nigeria imo… YES, yani hata ukizitaja tatu bora nayo
imo… Nigeria imetajwa kama nchi yenye uchumi mzuri mwaka 2015 na
yenyewe inashika nafasi ya tatu, wakati ya kwanza ni South Africa na ya
pili ni Egypt !!
Lakini kama unakumbuka vizuri, September
11 kila mwaka nchi ya Marekani ina kumbukumbu ya tukio la shambulio la
Kigaidi lililotokea New York, kwenye Jengo kubwa la Biashara la Kimataifa, World Trade Center mwaka 2001.
Baada ya kulipuliwa kwa Majengo ya kwanza, Marekani walijenga upya eneo hilo na huu ndio mwonekano wa sasahivi Majengo ya One World Trade Center, New York Marekani.
Sasa jina la World Trade Center linakuja Africa,
Mjengo unashushwa rasmi kabisa katikati ya Jiji la Abuja Nigeria… kitu
kitakuwa ni cha kisasa na ndani yake kutakuwa na vyumba vya Biashara
pamoja na apartments ambazo watapangishwa watu na watakuwa wanaishi kama
home tu yani !!
Moja ya Majengo ya World Trade Center ya Nigeria, Ujenzi umefikia hapa tayari.
Unaambiwa mpaka hiki kitu kikikamilika
kitakuwa kimeweka Rekodi ya kuwa Jengo kubwa zaidi Afrika Magharibi
ambalo ndani yake kuna shughuli za aina nyingi zinafanyika.
Mabadiliko makubwa yanatarajiwa kuonekana eneo hili mtu wangu, ndio ambapo World Trade Center inajengwa Nigeria.
Abuja itakuwa vizuri aisee, huu ndio mwonekano wa toka juu kitu cha World Trade Center kikikamilika.
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment