Watu 36 wameuawa
katika shambulio la kujitoa muhanga katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Ataturk Istanbul nchini Uturuki,na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa
Shughuli za usafirishaji katika uwanja huo zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma ya kwanza vikiendelea.. Mashuhuda wanasema waliwaona washambuliaji
watatu,ambapo mmoja kati yao alikuwa akifyatua risasi kabla ya kujitoa
muhanga kwa kujilipua kwa bomu na kufa.
Hata hivyo mashambulizi hayo yalihusisha katika eneo la kuingia katika uwanja huo.
Rais wa Uturuk Recep Tayyip Erdogan amelaani shambulio hilo na kusisitiza umoja katika kutokomeza vitendo hivyo.
Uturuki
imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya kigaidi kutoka pande
mbili,kwanza kutoka kwa kundi la Islamic State wanaoingia kutoka nchi
jirani ya Syria na waasi wa Kikurud wanataka kuunda dola yao.
BBC
No comments:
Post a Comment