El Chapo apinga kuhamishwa hadi Marekani
Mawakili wa mlanguzi huyo "El Chapo" wamepinga kuhamishwa kwake iliatumikie kifungo cha ulanguzi nchini Marekani baada ya kutoroka jela mara kadhaa akiwa nchini Mexico.
Mawakili wake wanadai kuwa hakuna ushahidi wa kumhusisha na njama ya kutoroka gerezani na wanakisia kuwa itachukuwa miaka 3 kwa kesi hizo kuamuliwa.
"El Chapo" anakabiliwa na mashtaka ya mauaji na ulanguzi wa mihadarati nchini Marekani.
"El Chapo" alikamatwa mwezi Januari takriban miezi 6 baada ya kutoroka gerezani akitumia njia ya chini kwa chini.
Uamuzi huo wa mahakama ya juu ni pigo kwa serikali hizo mbili na vita dhidi ya ulanguzi wa mihadarati.
BBC
No comments:
Post a Comment