Mbunge wa Leba auawa Uingereza
Mbunge wa chama cha
Leba nchini Ungereza Jo Cox ameaga dunia baada ya kupigwa risasi na
kuchomwa kisu akiwa kwenye mkutano katika eneo lake la ubunge kaskazini
mwa uingereza.
Cox Ndiye mbunge wa kwanza kuuawa nchini Uingereza tangu Ian Gow auawe mwaka 1990.Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 52 aliyetajwa na majirani kama mtu asiye na marafiki amekamatwa na silaha kupatikana.
Mtu mmoja aliyeshuhudia alisema risasi ilifyatuliwa wakati Bi Cox aliingilia kati.
Kisha muuaji akaanza kumchoma kisu alipokuwa amelala chini.
BBC
No comments:
Post a Comment