Mwandishi wa habari kahusishwa kwenye Ugaidi tena..
Mara nyingi waandishi wa habari wamekuwa
wakishutumiwa kwa kaucha taaluma zao na baadhi kujiingiza kwenye mambo
ya kisiasa kwa kuandika habari ambazo zina lengo la kupotosha jamii.
Hivi karibuni Waandishi wa habari kutoka
Misri walikaa kwenye Headlines kwa muda mrefu baada ya kuhukumiwa kwa
kosa la kushirikiana na kundi la Muslim Brotherhood na kuandika habari za kichochezi.
Stori nyingine iliyonifikia leo inatokea
huko Niger ambapo mwandishi wa habari mmoja ameshtakiwa kwa kosa la
kushirikiana na kundi la kigaidi la Boko Haram.
Waziri wa mambo ya ndani wa Niger alisema mwandishi huyo Moussa Tchangari amekuwa akishirikiana na kundi hilo la kigaidi na kueneza taarifa za uongo ambazo zilikua na lengo la kuchochea vurugu.
Pia amekuwa mstari wa mbele kuandika
habari zisizo za kweli kuhusu jeshi la nchi hiyo akidai lina makosa na
si Boko haramu huku mapema mwezi huu aliandika habari za kichochezi
kuhusu mapigano ya kundi la Islamic.
Hutopitwa n ahabari inayonifikia na nitakusogezea kila kinachonifikia kupitia hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment