Muuguzi tena kwenye headlines baada ya kuua wagonjwa wake…
Pamoja
na kazi ya uuguzi kuwa ni wito lakini kuna taarifa nyingi ambazo si
nzuri kwa wauguzi ambao hupewa jukumu la kuwahudimia wagonjwa lakini
wengine hutumia nafasi hiyo kutesa wagonjwa kwa kuwafanyia unyanyasaji.
Hii imetokea huko Uingereza ambapo muuguzi mmoja Victorino Chua wa hospitali ya Stepping Hills
amehukumiwa kwa kosa la kuwaua wagonjwa wake wawili na wengine 20
kuwawekea dripu yenye sumu kwa makusudi baada ya uchunguzi kukamilika.
Muuguzi huyo alisababisha vifo vya Tracy Arden, mwenye umri wa miaka 44, na Derek Weaver mwenye umri wa miaka 83 katika hospitali hiyo baada ya kuwazidishia dawa na mahakama kumfungulia kesi ya mauaji.
Imeelezwa
wagojwa hao waliwekewa sumu hiyo mwanzoni mwa mwaka 2011 na kufariki
July mwaka huo huo na hakuwa na mtu aliyehisi na sababu ya daktari huyo
kufanya hivyo haikufahamika na uchunguzi unaendelea.
Kwa habari na matukio motomoto ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment