Siku mbili baada ya tukio la Ijumaa, Watanzania hawa 35 Wamefikishwa Mahakamani

Ijumaa
kwenye taarifa kubwa kutoka taifa la Tanzania hii ya kituo kidogo cha
Polisi Bunju Dar es salaam kuchomwa moto na Wananchi kwa hasira ya
Mwanafunzi wa shule ya msingi kugongwa na gari barabarani ilikua
miongoni mwa habari kubwa July 10 2015.

Kwa
sababu walitoa malalamiko ya matuta kuwekwa na hayakuwekwa hivyo magari
yanapita kwa spidi zote, hasira zao walizimalizia kwa kuchoma moto na
kukiteketeza kabisa kituo cha Polisi.
Walifanikiwa kuvunja milango na wakaweka magurudumu na kukichoma moto
ambapo wakati wanafanya yote hayo ndani kulikua na mahabusu watatu
ambao walitolewa kuokoa maisha yao kabla ya moto kuwashwa.

Taarifa
rasmi za July 13 2015 ni kwamba Waliokamatwa kwa kuchoma moto kituo
hicho ni 35 na wamefikishwa Mahakamani na kusomewa mashitaka sita.
Kwa habari ,matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog.
No comments:
Post a Comment