Friday, July 10, 2015

BODABODA MUHEZA TANGA , WACHACHAMAA

Timu ya Tangakumekuchablog, Muheza

INADAIWA kutokea vurugu kubwa ya wafanyabiashara wa pikipiki maarufu kama (Bodaboda)  na polisi baada ya kutawanywa kwa mabomu ya machozi kwa kile kilichodaiwa kufanya maandamano ya kupinga mauaji ya bodaboda mwenzao kuuwawa kwa kutobolewa mcho.

Inadaiwa bodaboda huyo aliuwawa na watu wasiojulikna usiku wa kuamkia leo na kulazimika bodaboda vituo vyote ya Wilayani hapa kuandamana na hivyo kukutana na kigingi cha polisi baada ya kushindwa kutumia taratibu.

Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi jambo ambalo ilimelazimu shughuli nyingi za kijamii kusimama pamoja na wasafiri wanaoenda Mikoani kusubiri hamkani hiyo itulie.

Tanga kumekuchablog imefanya imemtafuta kamanda wa polisi Mkoa, Zubery Mombeji, lakini simu yake ya kiganjani  ilikuwa ikiita bila kupokelewa na ilipomtafuta Staff wake ilielezwa kuwa amenda eneo la tukio huko Muheza.

Kwa habari zaidi fuatilia blog hii itakuhabarisha kile kilichojiri kwa undani na ukweli pamoja na picha za tukio zima Muheza.

Kwa habari , matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment