MZEE OJWANG WA VITIMBI AFARIKI DUNIA JIJINI NAIROBI
Mwigizaji maarufu kutoka nchini
Kenya Mzee Ojwang amefaiki jana jumapili jioni katika hospitali
ya Kenyatta jijini Nairobi alikokuwa amelazwa , Mwigizaji Benson
Wanjau alisema Mzee Ojwang . alikuwa amelazwa hospitalini hapo
akisumbuliwa na ugonjwa wa Pneumonia. Ojwang alikuwa mwigizaji wa
vipindi maarufu vya Vitimbi, Vioja Mahakami, Vituko na Kinyonga katika
vituo vya luninga vya Kenya na ITV nchini Tanzania
Alijipatia umaarufu nchini Kenya
pamoja na maeneo yote ya nchi za Afrika Mashariki kutokana na uwezo wake
katika kuigiza ambapo alikuwa akiwavunja mbavu watazamaji wake kutokana
na vituko vyake na uwezo wake katika kuchekesha watazamaji wakati
akiigiza.
Tanga kumekucha itakusogezea kila kinachojiri ndani na nje ya nchi, ni hapa hapa
No comments:
Post a Comment