MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Uholanzi, Robin van Persie atajiunga na Fenerbahce
baada ya klabu hiyo kukubaliana na Manchester United leo.
Mkongwe
huyo mwenye umri wa miaka 31 anakwenda kufanyiwa vipimo England
kuelekea uhamisho huo wa Uturuki ambako atasaini Mkataba wa miaka mitatu
na kuwa na fursa ya kuongeza mwaka mmoja.
United
ilikataa kufikia makubaliano na Fenerbahce mwishoni mwa wiki baada ya
klabu hiyo ya Uturuki kutangaza nia ya kumsajili mchezaji huyo.
Van Persie anatarajiwa kuungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa United, Luis Nani, ambaye hivi karibuni amesaini Fenerbahce
Pamoja
na hayo, uhamisho huo sasa unathibitishwa baada ya kuwekwa wazi kwamba
mchezaji huyo hatakuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Louis van
Gaal Uwanja wa Old Trafford.
Na
Mholanzi huyo kwa kutaka kucheza michuano mikubwa ya Ulaya, ameichagua
timu ya Uturuki, ambayo wiki iliyopita ilimsajili winga wa zamani wa
United, Mreno Luis Nani.
Van
Persie aliyesajiliwa kutoka Arsenal, amebakiza mwaka mmoja katika
Mkataba wake Old Trafford na United imekubali kumuuza kwa Pauni Milioni
10.

No comments:
Post a Comment