Jeshi la Nigeria limewakamata hawa wengine waliojihusisha na Boko Haram!
Headlines za Boko Haram zinaendelea kusikika, ni kama vile wanapumzika kidogo alafu wanaibuka tena… Mpya kutoka Nigeria leo inawahusu baadhi ya watu waliokamatwa na Jeshi la Nigeria kwa mashtaka ya kuwa wao ndio waliokuwa wanahusika kupeleka mafuta ya petroli na bangi kwenye maficho ya Boko Haram.
Baadhi ya watu waliokamatwa wakijihusisha na vitendo vya kigaidi na Boko Haram.
Mkurugenzi wa Jeshi Mahusiano ya Umma Nigeria, Sani Usman alitoa kauli hiyo kupitia mtandao uitwao Prompt News Online, na kusema…
>>>
” Waalifu hawa ndio waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kupeleka
mafuta ya petroli, bangi na vilevi vingine … Jeshi la Nigeria
litaendelea kupambana kadri liwezavyo dhidi ya vitendo vya kigaidi
kwenye nchi hii ili kuhakikisha Nigeria inabaki salama na yenye amani…
Lakini hivi vyote vitakuwa vigumu kutimiza kama hatutakuwa na
ushirikiano kutoka kwa umma, tunakaribisha taarifa yoyote ile dhidi ya
matukio au mipango ya Boko Haram inayoendelea kwenye jamii “. <<< Sani Usman.
Mkurugenzi wa Jeshi Mahusiano ya Umma, Sani Usman amesema
hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu hao waliokamatwa
ambao kwa muda mrefu wamekuwa kikwazo cha amani sehemu mbalimbali nchini
Nigeria kwa kujihusisha na Boko Haram.
PAPO KWA PA
No comments:
Post a Comment