Thursday, September 10, 2015

UWANJANI HAKUNA UTOFAUTI KAZI NI MOJA TU

Messi ni mkali uwanjani, Luis Suárez ana beef? Majibu yake ni haya kuhusu ubora wa Messi…


Klabu ya Barcelona inajivunia Bonge la muunganiko wa Mastaa wao watatu wakali kabisa Uwanjani, Luis Suárez, Neymar na Lionel Messi… kila mmoja ana ubora wake na anakubalika, lakini nyota ya Lionel Messi inaonekana kung’aa zaidi, wenzake wanaichukuliaje?
Haya hapa ndio majibu ya Luis Suárez alipoulizwa jinsi anavyomchukulia Messi >>> ‘Hakuna mwenye wivu na mwenzake, sisi ni sehemu ya Kikosi na hakuna anayeshindana na mwenzake… kama ukiwa na Wachezaji wanaoshindana kila mmoja kuwa namba 1, lazima kuwe na matatizo. Niko kwa ajili ya kuisaidia Timu na sioni wivu‘ — Luis Suarez.
maxresdefault
September 09 2015 wamekutana Timu ya Taifa ya Mexico na Argentina, mechi ikaisha kwa goli 2-2… Hapa nina kipande cha video kinachomwonesha Messi alivyomtoka kipa wa Mexico pamoja na mabeki na kupachika goli.

No comments:

Post a Comment