Tangakumekuchablog
Tanga, BEI za
vyakula katika masoko Tanga
zimepanda maradufu na baadhi ya Masheikh kulazimika
kuzitumia mimbari zao kwa kuwaasa wafanyabiashara kutofanya hivyo kwa madai kuwa
ni makosa.
Hii inafuatia siku ya kwanza ya
mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuanza
vyakula katika masoko na maduka kupanda bei maradufu na wafungaji
kupatwa na kitisho cha ghafla.
Katika Soko kuu la Ngamiani,
Mgandini na Uzunguni bei za Nazi, mafuta, unga na baadhi ya vyakula vitumikavyo
kwa futari kupanda bei maradufu jambo ambalo masheikh kulazimika kuingilia
kati.
Imamu Mkuu wa Msikiti wa Quba,
Mohammed Abdullazizi, amewataka wafanyabiashara kuacha kuwalangua wafungaji na
kudai kuwa kufanya hivyo ni makosa na dhambi.
Amesema bei hizo zimewashtua wengi
na kulazimika kuingilia kati na kusema kuwa wataiomba tume ya kudhibiti bei
kuingia kati ili kuwapa unafuu wafungaji hasa kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa
Ramadhani
Mwisho
No comments:
Post a Comment