Tangakumekuchablog
Tanga,
WAFANYABIASHARA wa wenye maduka na sokoni Tanga wameaswa kutopandisha bei za
vyakula kipindi cha kuanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana, Kamishna wa NCCR Mageuzi Mkoa wa Tanga, Ramadhani Manyeko, alisema dalili
za awali zinaonyesha vyakula vitapanda bei maradufu.
Alisema kwa tathmini yake nazi, unga
na mafuta ambavyo hutumiwa kwa wingi kipindi cha mfungo vimepanda hivyo kuwapa
wakati mgumu wafungaji kipindi chote cha ssaumu.
“Nimefanya tathmini na kupitia
katika masoko na kugundua nazi unga na mafuta pamoja na sukari ambayo
tumeshazoea bei zake ziko juu maradufu, tukumbuke kuwa mwezi huo si wa ulanguzi
bali ni wa machumo wa kupata thawabu” alisema Manyeko na kuongoeza
“Kwanza maisha ni magumu halafu
mfanyabiashara kwa makusudi anawazidishia ukali wa maisha na saumu mfungaji kwa
tamaa tu ya kujipatia pesa kwa njia za kiulanguzi” alisema
Manyeko aliwataka wafanyabiashara
hao kwanza kumkumbuka Mungu katika biashara zao kwa madai kuwa utajiri hauwezi
kuwafikia kipindi cha Ramadhani pekee.
Alisema kipindi hiki cha mfumuko wa
bei ya sukari katika baadhi yaMikoa inaweza kuwaweka katika wakati mgumu
wafungaji kwani vyakula vingi vitumikavyo kama futari hutumia sukari.
Aliwataka wafanyabiashara hao kuacha
kupandisha bei na kuwapa nafuu wafungaji ikiwa na pamoja na kumuogopa Mungu kwa
kuongeza bei vyakula kipindi chote cha mfungo.
Mwandishi wa Tangakumekuchablog alitembelea
masoko ya Mgandini, Ngamiani, Makorora na Uzunguni na kubaini baadhi ya vyakula
kupanda bei ikiwemo Sukari, 2,400, Mahage, 1,700, Mchele 2,300 na n azi, 800 hadi 1,000.
Mwisho
No comments:
Post a Comment