Tetesi za soka Ulaya
Arsenal wataongeza
dau na kufikia pauni milioni 35 kumtaka mshambuliaji wa Lyon Alexandre
Lacazette, 25, baada ya dau la awali la pauni milioni 29.3 kukataliwa na
klabu hiyo ya Ufaransa (Daily Telegraph).
Arsenal pia wanataka
kumsajili beki wa Torino, Bruno Peres, 26, huku klabu hiyo ikitaka pauni
milioni 16.9 kulingana na (Gazzetta World).Vilevile klabu hiyo inazungumza na Valencia kutaka kumsajili beki mjerumani Shkodran Mustafi, 24, ambaye ana kipengele cha uhamisho chenye thamani ya pauni milioni 42.1 kwenye mkataba wake (Sky Sports).
Kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 24, amekataa kusaini mkataba mpya, kwa sababu anataka mshahara wake wa pauni 30,000 kwa wiki kuongezwa (Evening Standard).
Nayo Swansea wamepanda dau la kumtaka mshambuliaji wa Sevilla, Fernando Llorente, 31, baada ya Bafetimbi Gomis kwenda Marseille kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, na hivyo hawana mshambuliaji rasmi kwa sasa (Daily Mail).
Na hayo yakijiri Manchester United inakaribia kumsajili beki wa kulia kutoka Brazil anayechezea Monaco, Fabinho, 22 (globoesporte).
Aston Villa wanaonekana watamuuza Idrissa Gana, 26, huku Everton wakiwa tayari kukamilisha usajili wa pauni milioni 7.1 kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal (Daily Mirror). Vilevile beki wa Manchester United Cameron Borthwick-Jackson, 19, huenda akaondoka Old Trafford na kwenda kucheza kwingineko kwa mkopo (Manchester Evening News).
Everton wanataka kumsajili beki wa Swansea Ashley Williams, 31, ambaye huenda akagharimu pauni milioni 10 kwa mujibu wa (Daily Mirror).
Nayo
Klabu ya Galatasaray inataka kumsajili beki wa Manchester City Jason Denayer, 21, na pia kiungo wa Liverpool Lucas Leiva, 29 (Daily Mirror).
No comments:
Post a Comment